Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Gavana wa Benki kuu nchini (BOT), Emmanuel Tutuba amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa za kiuchimi kupitia sekta za kibenki ikiwemo nafasi za masomo na maswala ya kibenki, zinazotolewa na taasisi za kifedha nchini zikiwemo mabenki na makampuni mbalimbali ili kujiongezea uwezo wa kujitegemea.

Hayo ameyasema leo Aprili 2,2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mashindano ya TIOB (The Tanzania Institute of Bankers) kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka 2024.

Amesema kufuatia na mifumo imara iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya benki imepelelekea kuwa na mifumo mingi inayowezesha sekta binafsi kuweza kuingia na kufanya kazi vizuri na kupata faida.

“Tuwajengee uwezo vijana kuhusu maswala ya kifedha wakiwa bado wapo shuleni hii itasaidia watakapomaliza chuo waweze kujiajiri lakini pia kuajilika na itasaidia kuendelea kupunguza mikopo chechefu”, amesema Tutuba.

Amesema kufuatia hali ya uchumi kwa sasa katika sekta ya kibenki kwa asilimia 70 inaendesha na sekta binafsi hii inaamaana kwamba uchumi wa tanzania unaendesha na sekta binafsi

“Shughuli za uchumi zinaendelea kupanuka hivyo serikali imeweka mazingira huru ya kila mmoja kufanya shughuli zake kwa sasa ukiangalia product zote zinazingatia mifumo iliyo huru ambapo sekta binafsi zinaweza kuziendesha”,smesema.

Aidha Tutuba ameongeza kwa Kiwango cha mikopo chechefu imepungua kwani lengo lilikuwa kufikia chini ya asilimia tano lakini sasa imefikia asilimi 4 hivyo kama nchi inapaswa kujivunia kwa hili.

Amesema kwa namna ambavyo serikali inavyoshirikiana na mabenk wanaamini hiyo mikopo chechefu inaendelea kushuka zaidi huku tukihamasisha mabenki kwenda vijijini na kuwa na bidhaa ambazo zitawasaidia wote kutumia mabenki.

Akizungumzia kuhusu uhaba wa dola nchini amesema dola zipo na wanaendelea kulipia miradi yote ya serikali na hakuna mradi ambao umewahi kukwama au kuchelewa kwa sababu ya kukosa dola.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa TIOB Patrick Mususa amesema shindano hilo linalengo la kuelimisha vijana jinsi ya kutoa huduma za kifedha kwa kutumia mbinu bora.

Amesema mashindano hayo yamezinduliwa leo na yanatarajiwa kuisha Julsi 7, 2024 ambapo washindi watashida zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslim milioni tatu huku gavana akiahidi kuiongeza na kufikia milioni 5 kwa mshindi wa kwanza.

“Wanafunzi wote kutoka Taasisi za elimu ya juu wanaruhusiwa kushiriki wakati wowote popote walipo kwani shindano hili linaendesha kwa njia ya digitali kwa kutumia simu ya mkononi kwa kutumia Whatsapp kwa kutuma neno MENU kwenda namba 0763808776”, amesema Mususa.

Sambamba na hayo Mususa ametoa rai kwa taasisi mbalimbali za fedha kushirikiana na TIOB kuhakikisha wanaendelea kutoa motisha kwa wanafunzi kushiriki shindano hilo.

Please follow and like us:
Pin Share