Category: Siasa
Wakubwa wanavyotafuna Bandari
Majambazi wajitangazia Serikali
*Wajiundia Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo
*Wabuni bendera, mahakama na polisi yao
*Vijiji vyawatii, waendesha ujangili, ujambazi
Watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na majangili, wamejiundia serikali ndani ya Msitu wa Igombe mkoani Tabora, JAMHURI inathibitisha.
Wamejiundia uongozi madhubuti pamoja na jeshi walilolipa jina la Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa huenda idadi ya watu hao ikawa kubwa kuliko inavyodhaniwa, kwani wanadaiwa kusambaa ndani ya misitu minene katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Pia wapo katika maeneo kadhaa ya Mkoa wa Kigoma.
Imebainika kuwa watu hao wapo katika Msitu wa Igombe uliopo wilayani Uyui na kusambaa katika mapori mengine ya Malagarasi na Myowosi; na walianza kujiimarisha tangu mwaka 2010.
Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanaounda ‘serikali’ hiyo wanatoka katika makabila kadhaa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga, Arusha, Kigoma na katika mataifa jirani, hasa Burundi.
“Serikali” hiyo batili ina jeshi lake la ulinzi, jeshi la polisi, mahakama na vyombo vingine vya utawala.
Shughuli kuu zinazofanywa ni ujambazi, ujangili, kilimo cha bangi, biashara ya mbao, uuzaji bunduki pamoja na risasi; na uhalifu wa aina nyingine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, amezungumza na JAMHURI na kusema, “Ni kweli tuna tatizo hilo. Lipo na ni kubwa. Serikali imeshalitambua, na hatua zinachukuliwa.”
Mwasa, licha ya kukiri, hakutaka kuingia kwenye undani wa suala hilo katika kile kinachoonekana kuwa ni kutotaka kutibua hatua za kiusalama zilizopangwa kuchukuliwa na vyombo vya dola katika kukabiliana na genge hilo.
Hata hivyo, maneno ya Mwasa katika kuthibitisha ukubwa wa jambo hili ni haya, “Kweli tatizo lipo…ni kubwa kuliko unavyofikiri.”
Watu wawili waliokamatwa na baadaye kutoroka kutoka mikononi mwa kundi hilo wamesema genge hilo ni masalia ya wale walioshughulikiwa na Serikali mwaka 2010. Majina ya watu hao tunayahifadhi kutokana na sababu za usalama wao.
“Kuna jeshi lenye askari wa jadi wenye bunduki za SMG (Sub Machine Gun), na magobore. Wanaendesha uasi. Wamepandisha bendera ya bluu, imeandikwa Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo. Wahalifu wengi wageni wanatoka Burundi. Wanashirikiana na Wasonjo, Wasukuma na Waha.
“Shughuli zao ni kilimo cha bangi, kupasua misitu, uwindaji haramu na n.k. Wana watemi wao. Kila mtemi analindwa na askari wasiopungua 20,” anasema mmoja wa watoa habari wetu.
Uimara wa magenge hayo ya wahalifu yaliyojiimarisha yamewafanya hata wananchi na viongozi wa vijiji jirani na mapori wanamoishi, wawe watiifu kwao.
“Ukiwa na tatizo unaenda msituni kuomba msaada wa askari kukukamatia mhalifu au mbaya wako. Wanatumwa askari wanakuja kukuteka na kukupeleka huko msituni.
Nyalandu ‘auza’ Hifadhi
*Yeye, James Lembeli waenda Afrika Kusini kukamilisha mpango
*Baada ya Katavi Hifadhi nyingine nazo zitatolewa kwa wawekezaji
*Katibu Mkuu ashinikizwa, abaki njia panda kuidhinisha safari, malipo
*Urafiki wa Waziri, Lembeli waibua shaka miongoni mwa watumishi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, yupo kwenye hatua za mwisho za kuikabidhi Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa mwekezaji wa Afrika Kusini.
Bilionea Lake Oil kitanzini
*Yeye, wenzake wafungiwa vituo kwa kuchakachua *Walipa mamilioni ya shilingi Kampuni ya Lake Oil inayomilikuwa na bilionea Ally Awadh, imeingia matatani baada ya vituo vyake vinne vya mafuta kufungiwa kutokana na kuuza mafuta yasiyokuwa na vinasaba. Vituo vilivyofungwa ni Lake…
Ufisadi wa kutisha Mamlaka ya Ngorongoro
*Mapato ya Sh milioni 300 yaingia mifukoni *Safari hewa zagharimu shilingi bilioni 1.316 *Bia, soda, teksi vyagharimu Sh milioni 133 *Masurufu pekee yalamba shilingi milioni 100 Ufisadi wa kutisha umebainika kuwapo katika Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA), huku Serikali…
Pinda agongana na bilionea Dar
*Ni Ally Awadh wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil
*Atuhumiwa kumfanyia unyama mtumishi wake
*Polisi Oysterbay, Kanda Maalumu wamgwaya
[caption id="attachment_1591" align="alignleft"]Mlalamikaji anayedaiwa kupigwa na mabaunsa wa mfanyabiashara bilionea Ally Awadh (Lake Oil)[/caption]Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua “kujipima uzito” dhidi ya bilionea Mtanzania, Ally Edha Awadh ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam inayoagiza, kuuza na kusafirisha mafuta na biashara nyingine nyingi.
Awadh anayetajwa kama mmoja wa mabilionea vijana nchini, amefunguliwa mashitaka Polisi ya kumteka, kumdhalilisha kinyume cha maumbile na kumpora mali mmoja wa wafanyakazi wake.
Uamuzi wa Waziri Mkuu Pinda umekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini, katika kile kinachoonekana ni kumgwaya bilionea huyo, kupuuza kumsaidia mlalamikaji huyo mwenye umri wa miaka 32. Kwa sababu za kiutu na za kitaaluma, jina la mlalamikaji tunalihifadhi kwa sasa.
- Serikali itaendelea kuiamini na kuiunga mkono Red Cross – Dk Biteko
- Dk Biteko ashiriki Tulia Marathon Mbeya
- Makala : Changamoto za barabara Ulanga na Malinyi zitafanyiwa kazi
- Tanzania, DRC kukuza uchumi kupitia bandari
- Mwalimu aliyejipatia mafao kutoka PSSF milioni 70.3 kwa udanganyifu aenda jela miaka 65
Habari mpya
- Serikali itaendelea kuiamini na kuiunga mkono Red Cross – Dk Biteko
- Dk Biteko ashiriki Tulia Marathon Mbeya
- Makala : Changamoto za barabara Ulanga na Malinyi zitafanyiwa kazi
- Tanzania, DRC kukuza uchumi kupitia bandari
- Mwalimu aliyejipatia mafao kutoka PSSF milioni 70.3 kwa udanganyifu aenda jela miaka 65
- TMA yatoa tahadhari ya matarajio ya hali ya hewa mbaya kwa siku tano
- Weather forecast for the next 24 hours
- Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Simanjiro afikishwa mahakamani kwa rushwa
- Rais Dk Samia aagana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Chapo
- Kapinga azindua kituo mama cha gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) Dar
- Shirika la Posta Tanzania lashiriki kongamano la eLearning Afrika, laja na huduma ya Swifpack
- Matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030 – Dk Biteko
- Wajumbe, mabalozi 2,200 wanufaika na mafunzo ya utatuzi wa migogoro Songea
- Papa aongoza misa kwa mara ya kwanza
- Papa Leo XIV apokelewa kwa matumaini Congo