TEF yapata safu mpya ya uongozi

Mhariri Mtendaji wa Gazeti JAMHURI, Deodatus Balile, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Balile alichaguliwa katika nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mjini Morogoro. Katika uchaguzi huo uliojaa ushindani, Balile alipata kura 47 na kumshinda Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu, aliyepata kura 17 kati ya kura…

Read More

Ya Lake Oil tuliyasema

Februari, 2013 tuliandika habari ambayo hatimaye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, imeuthibitishia umma ilikuwa kweli. Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil imebainika kukwepa kodi ya Sh bilioni 8.5 kwa kufanya udanganyifu kwenye biashara ya mafuta kwa kutumia kivuli cha usafirishaji nishati hiyo nje…

Read More

Mabadiliko Bandari

Baada ya Bandari ya Dar es Salaam kulalamikiwa kwa muda mrefu kuwa haina ulinzi mzuri wa mali za mateja, hatimaye uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) umechukua hatua za dhati kwa kuimarisha mfumo wa ulinzi. Kati ya mambo waliyofanya, ni pamoja na kuanza kufunga kamera za usalama (CCTV) zipatazo 486 ambazo sasa zinamulika Bandari…

Read More

Ukweli kuhusu UDA

Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), Robert Kisena alikutana na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam akazungumza nao kuhusiana na habari kuu tuliyoichapisha katiak toleo Na 225 la Gazeti la JAMHURI. Katika maelezo yake, alikanusha habari tuliyoichapisha ukurasa wa kwanza iliyosema “Familia ya Kikwete inahusika UDA.” Katika habari hiyo,…

Read More

Prof. Lipumba atia ubani Zanzibar

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekuwa sehemu ya makundi ya watu wa kada mbalimbali nchini anayepinga kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. “Zanzibar inaumbiwa hatari kubwa, na mtu wa kuokoa hatari hiyo si mwingine. Ni Rais Dk. John Pombe Magufuli. Nina imani na Rais Magufuli anaweza kulitatua hili kwa matokeo…

Read More

Bodaboda waomba kumuona Rais Magufuli

Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda jijini Dar es Salaam wamesema wananyanyasika kupita kiasi kutokana na kukamatwa hovyo na askari na watu wasiofahamu ni kina nani, hivyo wanaomba Rais John Magufuli aingilie kati kuwaokoa. Wakizungumza na JAMHURI mwishoni mwa wiki, wadereva hao wa pikipiki wamesema tofauti na ahadi ya Rais Magufuli kuwa wasibugudhiwe, mateso na manyanyaso…

Read More