JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

Bandari Dar inakufa

*Mkurugenzi Mkuu Kipande aingiza ukabila, udini, majungu

*Wafanyakazi watatu bandarini wafariki kutokana na vitisho

*CCTV hazifanyi kazi tangu 2011, wachonga dola mil. 6.5

*Mnikulu Gurumo, Mtawa wampa kiburi, wachafua jina la JK

*Amdanganya Dk. Mwakyembe, amtukana Balozi wa Japan

Kuna kila dalili kuwa Bandari ya Dar es Salaam inakufa kutokana na uongozi mbovu uliojiingiza katika majungu, udini, ukabila na majivuno yasiyo na tija. Wafanyakazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamepoteza morali wa kufanya kazi kutokana na vitisho na matusi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Madeni Juma Kipande.

Hadi habari hii ya kiuchunguzi inachapishwa wafanayakazi watatu; Peter Gwamaka Kitangalala, Dotto Mbega na mwingine aliyefahamika kwa jina la Lyochi wamefariki dunia katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na shinikizo la damu lililozaa kiharusi baada ya vitisho vya Kipande.

Katika hali ya kuwavuruga wafanyakazi wa bandari, Katangalala alihamishiwa Mwanza na baada ya miezi miwili akahamishwa tena kwenda Lindi, huku akipewa vitisho kuwa muda wowote ajiandae kufukuzwa kazi. Kutokana na hofu, alipata kiharusi (stroke) akafa. Mbega kwa upande wake yeye alikuwa makao makuu Dar es Salaam, lakini kutokana na vitisho vya kila siku vya Kipande na wasaidizi wake, naye akapata kiharusi mwezi mmoja uliopita akafariki dunia.

Jumapili ya Machi 30, mfanyakazi mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Lyochi huku wengine wakisema ni Oluwochi mwenye asili ya Wajaruo, aliyehamishiwa bandari ya Kasanga, Sumbawanga naye aliaga dunia kwa ugonjwa huo huo wa kiharusi kutokana na mashinikizo ya Kipande.

“Uhalisia hali inatisha. Kipande anajinadi kuwa atamfukuza kila mtu, na kweli anafukuza anaajiri watu wa dini yake. Kuna kabila la Wahaya kutoka Kanda ya Ziwa, hilo utadhani waliwahi kushikana nalo ugoni. Mhaya yeyote aliyemkuta kazini ameapa kumg’oa. Amehamisha [Hassan M.] Kyomile kwa sababu ya kabila lake na kwamba aliomba kazi ya Ukurugenzi Mkuu,” kilisema chanzo chetu.

Kyomile amehamishwa Machi mwaka huu, kutoka makao makuu alikokuwa Mkurugenzi wa Ununuzi na kwenda kuwa Meneja wa Bandari Tanga.

Nyalandu ‘auza’ Hifadhi

*Yeye, James Lembeli waenda Afrika Kusini kukamilisha mpango 

*Baada ya Katavi Hifadhi nyingine nazo zitatolewa kwa wawekezaji

*Katibu Mkuu ashinikizwa, abaki njia panda kuidhinisha safari, malipo

*Urafiki wa Waziri, Lembeli waibua shaka miongoni mwa watumishi

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, yupo kwenye hatua za mwisho za kuikabidhi Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa mwekezaji wa Afrika Kusini.

Bilionea Lake Oil kitanzini

*Yeye, wenzake wafungiwa vituo kwa kuchakachua *Walipa mamilioni ya shilingi Kampuni ya Lake Oil inayomilikuwa na bilionea Ally Awadh, imeingia matatani baada ya vituo vyake vinne vya mafuta kufungiwa kutokana na kuuza mafuta yasiyokuwa na vinasaba. Vituo vilivyofungwa ni Lake…

Ufisadi wa kutisha Mamlaka ya Ngorongoro

  *Mapato ya Sh milioni 300 yaingia mifukoni *Safari hewa zagharimu shilingi bilioni 1.316 *Bia, soda, teksi vyagharimu Sh milioni 133 *Masurufu pekee yalamba shilingi milioni 100 Ufisadi wa kutisha umebainika kuwapo katika Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA), huku Serikali…

Pinda agongana na bilionea Dar

*Ni Ally Awadh wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil
*Atuhumiwa kumfanyia unyama mtumishi wake
*Polisi Oysterbay, Kanda Maalumu wamgwaya

[caption id="attachment_1591" align="alignleft"]Mlalamikaji anayedaiwa kupigwa na mabaunsa wa mfanyabiashara bilionea Ally Awadh (Lake Oil)[/caption]Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua “kujipima uzito” dhidi ya bilionea Mtanzania, Ally Edha Awadh ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam inayoagiza, kuuza na kusafirisha mafuta na biashara nyingine nyingi.

Awadh anayetajwa kama mmoja wa mabilionea vijana nchini, amefunguliwa mashitaka Polisi ya kumteka, kumdhalilisha kinyume cha maumbile na kumpora mali mmoja wa wafanyakazi wake.

Uamuzi wa Waziri Mkuu Pinda umekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini, katika kile kinachoonekana ni kumgwaya bilionea huyo, kupuuza kumsaidia mlalamikaji huyo mwenye umri wa miaka 32. Kwa sababu za kiutu na za kitaaluma, jina la mlalamikaji tunalihifadhi kwa sasa.

Kitanzi cha JK

Wizara ya Maliasili yatajwa kuwa mtego kwa Kikwete

Pinda, Mwamunyange, Mwema watakiwa kupima uzito

Rais Jakaya Kikwete, akiwa anatarajiwa kulisuka upya Baraza la Mawaziri, kuna kila dalili kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa sasa ndio imebaki kuwa kitanzi kinachotishia uhai wa Serikali yake.