Category: Kitaifa
Sakata la Iddi Simba bado bichi
*Ikulu, ofisi ya CAG washangazwa kuachiwa
*Uamuzi uliofanywa na DPP wazua maswali
Kuachiwa kwa mwanasiasa Iddi Simba, ambaye hivi karibuni alikuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kabla ya Mkurugenzi wa Mshitaka nchini (DPP), kuamuru awe huru, kumeibua mgongano mkubwa serikalini.
Obama atoboa siri
*Aeleza anavyokunwa na kazi nzuri inayofanywa na Tanzania
*Amsifia Rais Kikwete, aunga mkono Jeshi la Tanzania Congo
*Aeleza wazazi wake walivyoishi Tanzania, JK aishukuru USA
Rais Barack Obama wa Marekani ametua nchini na kupokewa kwa kishindo na kutoboa siri ya anayojua juu ya Tanzania, huku akieleza kuguswa na mapokezi ya aina yake.
Utajiri wa Obama Sh bilioni 32
Dhana kwamba wanasiasa wanapaswa kuwa watu maskini huenda imepitwa na wakati. Rais wa Marekani, Barack Obama yeye na familia yake wanamiliki utajiri wa dola 19,225,070 sawa na Sh 31,529,114,800.
Ujio wa Obama wabadili mfumo Dar
Ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, hapa Tanzania imebadili mfumo mzima wa matumizi ya barabara na shughuli mbalimbali jijini Dar es Salaam.
PPF yazidi kuchanja mbuga
Mfuko wa Pensheni za Mashirika ya Umma (PPF) umetangaza kuongeza fao la elimu kuanzia kidato cha nne hadi cha sita, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 35 ya mfuko huo.
Wahadhiri TEKU watangaza mgomo
Hali si shwari ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), baada ya uongozi wa Chama cha Wahadhiri wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufunga mhula, inayotarajiwa kufanyika Julai mosi, waka huu.