Category: Kitaifa
Ridhiwani Kikwete aanika utajiri wake
*Aeleza adha za kuwa mtoto wa Rais, ataja fedha alizonazo benki
*Azungumzia urais 2015, uhusiano wake na Membe, Lowassa
*Achambua mgogoro wake na Hussein Bashe, Dk. Wilbrod Slaa
Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, amefanya mahojiano maalum na Gazeti la JAMHURI nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, Machi 30, mwaka huu, na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu yeye binafsi na mengine yanayolihusu Taifa.
Mabadiliko ya kiuchumi yanukia Afrika
Mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kiuchumi yanatarajiwa kuonekana Afrika, amesema Katibu Mtendaji wa Baraza la Uchumi Afrika, Dk. Carlos Lopes.
Serikali, wananchi wahimizwa kuwajibika
Shirika la Forum Syd Tanzania limeihimiza Serikali kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo, na ameitaka na jamii yenyewe kuhakikisha inawajibika ili kuweza kukabili changamoto za umaskini wa kipato.
Arusha yazizima
Vifo visivyotarajiwa vya wafanyabiashara maarufu wawili – Henry Nyiti na Nyaga Mawalla – vimeibua hisia tofauti miongoni mwa wakazi wa Arusha na mikoa ya kaskazini kwa jumla. Nyiti alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni iliyojihusisha na uchimbaji na uuzaji vifaa vya madini ya Interstate Mining and Mineral,s iliyokuwa na makazi yake mkoani Arusha.
Lwakatare alivyorekodiwa
Taratibu mambo yameanza kuwekwa hadharani, na sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasema Mkurugenzi wao wa Idara ya Ulinzi, Wilfred Lwakatare, alirekodiwa na msaidizi wake, Joseph Ludovick. Hata hivyo, wakati Chadema wakiibua hayo, wanasema wanao ushahidi mzito unaonesha kuwa Ludovick alirubuniwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, kufanya uharamia huo.
‘Tumieni vyakula asilia’
Jamii imeshauriwa kujenga mazoea ya kutumia vyakula asilia, vikiwamo mbogamboga na matunda kupunguza kemikali, kutibu magonjwa na kusafisha damu mwilini.