JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Kuwafutia leseni hakutoshi, washitakiwe

Mojawapo ya habari zilizobeba uzito katika gazeti hili ni ile inayohusu uchakachuaji wa mbolea, ambao umekuwa ukichangia kudhoofisha juhudi za wakulima katika kujiondolea umaskini.

Polisi wazingatie mambo haya

Vyombo vya habari vimeandika na kutangaza juu ya matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi na vyombo vingine vya usalama nchini. Wadau mbalimbali wamejitokeza kulaani kifo cha mwandishi Daudi Mwangosi ambacho tunadiriki kusema wazi kwamba kimesababishwa na bomu lililofyatuliwa na mmoja wa polisi.

Sumatra na porojo za kujikosha

Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) inapendekeza kuwapo kwa kanuni kadhaa zinazolenga kupunguza ajali nchini. Katika mapendekezo hayo, Sumatra wanataka umri wa madereva wa magari ya abiria uwe kati ya miaka 30 hadi 60. Wamejikita kwenye hoja hiyo dhaifu kwa imani kwamba vijana chini ya umri wa miaka 30 ndiyo chanzo kikuu cha ajali za mabasi nchini!

Bila kuheshimu Katiba tutayumba

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwapo mjadala mkali kuhusu uhalali wa baadhi ya majaji na sifa zao za kuifanya kazi hiyo. Kumekuwapo madai kwamba baadhi ya majaji wameteuliwa ilhali wakiwa na rekodi mbaya za uombaji rushwa, uonevu, upendeleo na kukosa uadilifu.

Serikali iwanusuru mabalozi wetu

Katika toleo la leo tumechapisha taarifa zenye kuonyesha kuwa hali ya kifedha ya Balozi za Tanzania nje ya nchi ni mbaya. Habari hizi zinaonyesha kuwa Balozi karibu zote zinakabiliwa na madeni, zimekatiwa huduma za simu, maji, umeme na mifumo ya…

Madai ya Tundu Lissu yachunguzwe

Katika gazeti la leo kuanzia ukurasa wa kwanza tumechapisha ripoti maalum yenye kuonyesha hali ya wasiwasi katika muhimili wa tatu wa dola uliokasimiwa jukumu la msingi la kutoa haki. Wasiwasi huu umeibuliwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge.