JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Anwani za makazi, vitambulisho vya taifa vina umuhimu wa pekee

Katika toleo la leo tumechapisha habari za mchakato wa kuandaa anwani za makazi (postal code) kukamilika. Mpango huu umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na muda si mrefu karibu kila nyumba hapa nchini itakuwa ikitambulika.

Waziri makini hawezi kusherehekea uteuzi

Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika Baraza la Mawaziri. Baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri wamepoteza nafasi walizokuwa wakishikilia, kutokana na kashfa ya ufujaji wa fedha na mali nyingine za umma.

Tanzania si nchi masikini, wafanyakazi walipwe vizuri

Leo ni Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani. Tunawapongeza wafanyakazi wa Tanzania ambao, licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu na kupata ujira mdogo, wameendelea kuwa wavumilivu.

Uvamizi huu unafanywa viongozi wakiwa wapi?

Kwa siku kadhaa sasa mamlaka katika Jiji la Dar es Salaam zimekuwa zikiwahamisha wachuuzi waliovamia hifadhi za barabara na kuendesha biashara. Vurugu zimeripotiwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya Ubungo na mengine jijini humo.

Hongera Nassari, hongera Chadema

Wapigakura wa Arumeru Mashariki wameamua. Wamemchagua mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari kuwa mbunge wao. Nassari amewashinda wagombea wengine saba wa vyama vya siasa, akiwamo Sioi Sumari aliyekuwa akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).