Category: Siasa
Vilivyobakia ardhi na watu
Siku zilizopita katika Safu hii, niliwahi kuzungumzia Azimio la Arusha, dira iliyoaminika ingewapeleka na kuwafikisha Watanzania kwenye Ujamaa kamili chini ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Kwa kweli kwa miaka ile ya kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1990, Azimio lilistahili kuwapo, kwani nchi ilikuwa katika harakati za ukombozi; ukombozi wa kiafikra, kisiasa, kiuchumi, kiutawala na kiutamaduni.
Safari hii ya Goma ihitimishiwe Kigali
Meja Khatibu Mshindo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amekufa katika mapambano nchini DRC. Amekufa kishujaa. Amekufa akitekeleza maelekezo halali ya Umoja wa Mataifa (UN) yanayolenga kuwafanya wananchi wa Mashariki mwa DRC waonje tunu ya amani. Kifo cha kamanda huyu kinapaswa kiwe chachu kwa Watanzania na wapenda amani katika Afrika na duniani kote.
Bashar al-Assad: Mbabe anayeitikisa Dunia
Kwa zaidi ya miezi kumi nchi ya Syria imeingia katika mzozo uliosababisha machafuko makubwa nchini humo na kusababisha watu zaidi ya 1300 kupoteza maisha. Mzozo huo unasababishwa na wananchi wa nchi hiyo kutoikubali serikali inayongozwa na Rais Bashar al-Assad.
KAULI ZA WASOMAJI
Daraja la Mbutu vipi?
Pongezi kwenu waandishi wa Gazeti JAMHURI kwa kutujulisha habari zenye weledi. Kero yangu ni ujenzi wa daraja la Mbutu. Kasi ya ujenzi wa daraja hili umekuwa wa kusuasua, na masika karibu yanaanza. Jamani mnaohusika na ujenzi huu fanyeni haraka kuukamilisha
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Kujidai unajua kila kitu ni hatari
“Kiongozi anayejidai kuwa anajua kila kitu, na kumbe hajui, ni hatari zaidi kuliko yule anayekiri kuwa hajui kitu na yuko tayari kujifunza.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Alizaliwa 1922, akafariki 1999.
Yah: JWTZ kuwa ya kivita zaidi, siyo mbwembwe
Nawapa hongera wale wote tuliotoa michango yetu ya hali na mali mwaka 1978 hadi 1980 wakati wa vita ya kumtoa yule jamaa wa Uganda aliyekuwa na mbwembwe nyingi za maneno na vitendo. Kuna wakati, kwa akili yake ya kuvukia barabara, alitaka wakutane na Julius ulingoni wachapane makonde, hiyo ndiyo akili ndogo katika kichwa kikubwa.