Category: Siasa
Migiro hakuhujumu mchakato wa katiba
Kama tujuavyo, Watanzania tuko katika mchakato wa kutafuta Katiba mpya ya nchi yetu. Katika kipindi hiki, vyama vya siasa vinatoa maoni mbalimbali kuhusu mchakato huo. Nacho Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakikubaki nyuma.
Kwanza niwapongeze ndugu zetu wa Chadema kwa mafanikio makubwa wanayopata katika kukusanya nyaraka nyeti.
Miundombinu duni inachangia umaskini
Miundombinu (Infrastructures) duni inachangia kukuza umaskini wetu. Watu wanazidi kuwa maskini kwa vile miundombinu iliyopo haileti unafuu wa kupunguza gharama za usafiri kwa abiria na mizigo.
Sisi Waafrika weusi tukoje? (5)
Ili Waafrika weusi sisi tupate maendeleo katika nchi zetu, hatuna budi kujitafiti na kujitambua upungufu wetu wote. Upungufu wa kutamani kuwa kama Mzungu au Mwarabu haujaondoka katika fikra zetu ingawa wakoloni hawapo; lakini kwa mazoea yetu sisi Mzungu ni wa kuogopwa tu.
KAULI ZA WASOMAJI
Serikali isiwadhulumu wastaafu
Ukweli ni kwamba ni laana kubwa kwa Serikali kudhulumu malipo ya fedha za wazee wastaafu, walioitumikia nchi hii katika nyanja mbalimbali.
Msomaji
* **
NUKUU ZA WIKI
Nyerere: Umaskini wa fikra mbaya sana
“Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo (fikra), ni umaskini mbaya sana. Mtu mwenye akili akikwambia neno la kipumbavu ukalikubali, anakudharau.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
***
Lissu: Tume ya Katiba ni ulaji
*Asema wanatumbua fedha, watengewa fungu la Ukimwi
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, wiki iliyopita aliwasilisha bungeni maoni ya Kambi hiyo, na kueleza namna Tume ya Mabadiliko ya Katiba inavyofuja fedha.