Serikali isiwadhulumu wastaafu

Ukweli ni kwamba ni laana kubwa kwa Serikali kudhulumu malipo ya fedha za wazee wastaafu, walioitumikia nchi hii katika nyanja mbalimbali.

Msomaji

* **

Viongozi mnatuumiza wananchi

Viongozi wawajibike kukidhi mahitaji ya wananchi, si kujinufaisha wao binafsi (ninaona kwamba viongozi mnatuumiza wananchi).

Misana Maalim

Mbagala, aDar es Salaam

***

 

Waliostaafu zamani wanapunjwa

Malipo ya pensheni kwa watumishi wa umma waliostaafu zamani, ni kiduchu ikilinganishwa na ya waliostaafu hivi karibuni, wakati soko la kununulia mahitaji ni moja. Usawa uko wapi hapa?

Mtanzania Mzalendo

***

 

PSPF hatarini kufilisika

Mimi ni mdau wa PSPF tangu mwaka 2005. Naona kwamba mfuko huu unaelekea kukabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa. Sipati picha.

Mdokezaji

Dar es Salaam.

***

 

Dampo la Bomang’ombe kero

Kilio chetu wakazi wa eneo la Bomang’ombe wilayani Hai, ni dambo linalotukera na kuhatarisha afya zetu. Tumelalamika lihamishwe lakini wahusika hawatusikilizi.

Mkazi wa mjini Hai

***

 

Hongera Gazeti JAMHURI

Nawapongeza watendaji wote wa Gazeti la JAMHURI, kwa juhudi zenu za kuihabarisha jamii. Tunatarajia habari na makala nzuri zaidi kwenye gazeti hili kwa manufaa ya umma.

Mchangiaji.

***

 

Viongozi muwe na huruma

Viongozi mliopewa mamalaka ya kuwahudumia wananchi muwe na huruma. Wananchi wa Kata ya Mwangemshindo, Manispaa ya Songea mmetaka ardhi na nyumba zao na kuzifanyia  tathmini mwaka 2008, kwa nia ya kuwapa EPZ lakini hadi leo hawajalipwa. Kitendo hicho ni cha kulaaniwa kabisa. CCM mnaiweka majaribuni kwa wananchi.

Mwananchi Songea.

***

 

Serikali imeshindwa kubomoa maghorofa

Serikali imeshindwa kushinikiza kubomolewa kwa maghorofa yasiyokidhi viwango, au inasubiri idadi  fulani ya watu wafe ndipo wachukue hatua?

David Mayala,

Biharamulo, Kagera

***

 

Viongozi watumie uongozi wao kukidhi haja za wananchi wao  si kujinufaisha wao (viongozi mnatuumiza wananchi).

Msomaji wa JAMHURI

***

 

RC Arusha ahamishwe

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ahamamishwe kwa kuwa huleta uhasama usio na tija kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Gobless Lema, hivyo kuzorotesha maendeleo na kujenga malumbano na kuwagawa wananchi. Hivyo, ili kupata utulivu, mkuu wa mkoa huyo ahamishiwe mkoa mwingine.

Msomaji wa JAMHURI,

Arusha

***

 

Mulugo ni mbabe

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, ni tabia yake ya kuwa mbabe na mtu wa kufanya mambo tofauti na cheo chake Akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kumtetea Afisa Usalama mmoja katika kugombea ardhi na mwanakajiji wa Mapinga, alidirikia kushiriki kamatakamata siku ya Jumapili, Mulugo yupo kwa maslahi ya waliomteua na marafiki zao na si kwa maslahi ya wananchi.

Mwanakijiji Mapinga,

Bagamoyo.

Please follow and like us:
Pin Share