Nyerere: Umaskini wa fikra mbaya sana

“Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo (fikra), ni umaskini mbaya sana. Mtu mwenye akili akikwambia neno la kipumbavu ukalikubali, anakudharau.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

***

Nooyi: Ni vigumu kuufafanua uongozi

“Ni vigumu kuufafanua uongozi, na ni vigumu zaidi kuufafanua uongozi bora, lakini kama utapata watu wa kukufuata hadi mwisho wa dunia, wewe ni kiongozi mkuu.”

Haya yalisemwa na Indra Nooyi, Mhindi-Mmarekani, mfanyabiashara, Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Pepsi inayofanya biashara za chakula na vinywaji duniani.

***

 

Mkuchika: Mafao ya wastaafu ni janga

“Mafao ya wastaafu ni kero kubwa ambayo watumishi wa umma hawana budi kuiondoa, mimi ninaifananisha na janga.”

Hii ni kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika.

***

 

Lagarde: Sekta ya fedha ni huduma

“Sekta ya fedha ni sekta ya huduma. Inapaswa kuwahudumia wengine kabla ya kujihudumia yenyewe.”

Kauli hii ni ya mwanasheria maarufu wa nchini Ufaransa, Christine Lagarde, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

 

Please follow and like us:
Pin Share