Category: Makala
Mkurugenzi: Wananchi Bukoba tulieni
*Asema ripoti ya CAG itatoa mwelekeo*Pande zinazovutana zaandaa ‘bakora’ Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Limbakisye Shimwela, amewaomba wakazi wa Manispaa hiyo kuwa watulivu na kusubiri majibu yatakayotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) baada ya ukaguzi…
Madudu ya Msekwa yaanikwa Ngorongoro
*Aliunda Kamati ikawa ndiyo Menejimenti
*Murunya naye ahusishwa kufaidi mabilioni
*Wameuza hadi mapitio ya wanyamapori
*Faru wengine watatu hawajulikani waliko
Timu ya ukaguzi iliyoundwa kukagua ‘madudu’ katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanika ufisadi wa kutisha, JAMHURI inathibitisha. Spika wa zamani, Pius Msekwa, ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao ripoti hiyo imependekeza wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Msekwa ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo inayosifika kwa ufisadi.
Yah: Sasa ndiyo nawakumbuka waliokuwa viongozi wazalendo
Huwa naona kama naota ndoto nzito, ambazo hazina mwisho kila ninaposikia vioja vya watendaji wa Serikali yetu katika kulitendea haki Taifa hili.
Napata taabu kukubaliana kama hawa ndiyo viongozi tuliowapigia kura ama walichaguliwa na Mungu, kuja kutuhukumu tungali hai kama vile mwisho wa dunia umefika.
IRENE DAVID: Binti aliyejiajiri kuuza matunda Dar
IRENE DAVID:
Binti aliyejiajiri kuuza matunda Dar
. Alikataa kutoa rushwa ya ngono aajiriwe
. Awaasa mabinti, wanawake wanaojiuza
Ni binti mrefu wa wastani, mwenye rangi ya maji ya kunde na umri wa miaka 23. Ni mhitimu wa kidato cha nne na fani ya kompyuta ngazi ya cheti, aliyejiajiri kuuza matunda. Binti huyu si mwingine yeyote bali ni Irene David, mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam. Ana kawaida ya kutabasamu anapozungumza na mtu.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
‘Kutegemea kubaya kupita kote ni kutegemea mtu mwingine kwa mawazo
Katika sehemu iliyopita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema hata angekuwa anafuata sera za kibepari, angejenga viwanda. Anasema mabepari ndiyo walioanza kujenga viwanda, na viwanda vyenyewe havikuwa na sera. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mwalimu aliyoitoa katika kilele cha Sherehe za Mei Mosi, mwaka 1995 mkoani Mbeya.Juzi
Rais Kagame si wa kumwamini sana
Makala iliyopita ya “JWTZ nginjangija Goma hadi Kigali’, imenifumbua macho. Nimepata simu nyingi na ujumbe wa maandishi usio idadi. Wapo waliotumia lugha kali, lakini wengi walikuwa waungwana. Hiyo ndiyo raha ya mijadala. Kuna wakati tunaweza kukubaliana kwenye baadhi ya mambo, na wakati mwingine tusikubaliane kwa hoja fulani fulani. Muhimu ni kujenga moyo wa uvumilivu na staha.