Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dodoma, Aisha Saleh Madoga, amejivua wadhifa wake na nafasi nyingine zote alizokuwa anazishikilia ndani ya chama hicho.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dodoma leo, Madoga amesema amejiuzulu kwa hiari yake kutokana na kile alichokieleza kuwa ni kushindwa kutekeleza majukumu kwa ufanisi wa kiwango anachokitamani.

“Siwezi kuendelea kuwaambia watu haya ni matatizo wakati siwezi kuyatatua. Niliamua kujiunga na CHADEMA kwa sababu naamini sauti yangu inaweza kusikika,” amesesema Madoga kwa hisia.