Diwani wa Kata ya Namichiga kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani Ruangwa mkoani Lindi Bwana, Mikidadi Ibadi Mbute, amejiuzulu nafasi yake na kutangaza kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Pia Bakari Hamisi Mpanya maarufu kama Selenge aliyekuwa Diwani wa Kata ya Nachingwea, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amejiunga na CCM na kusema ameridhishwa na kasi ya mbunge wa Ruangwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Please follow and like us:
Pin Share