Chalamila ataka kasi ya usambazaji majisafi Dar

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Septemba 22, 2023 katika muendelezo wa ziara yake Wilaya ya Kigamboni kukagua ufanisi wa uzalishaji wa maji Safi katika Mkoa huo, jukumu linalotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

Ameridhishwa na kiwango cha uzalishaji maji katika Mkoa ambapo takribani lita milioni 590 zina zalishwa kwa siku wakati mahitaji halisi ni lita Milioni 540 ” Kwa takwimu hizo tunaziada ya maji ninachokitaka sasa ni kazi kubwa ya Usambazaji wa maji kwa jamii tena uanze mara moja kwa mitaa 11 ya wakazi wa kisarawe II na kwingineko katika Mkoa huu” Amesema RC Chalamila.

Matarajio makubwa ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona maji yana mfikia kila mtu katika nyumba yake na sio kuwa na tenki kubwa la maji karibu lakini watu au jamii haina maji hiyo sio Sawa ni lazima katika utumishi wa umma kila mtu atekeleze wajibu wake

Aidha Mhe Chalamila akiwa Kigamboni amejionea mtambo wa kusukuma maji vilevile ametembelea tenki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi maji safi lita milioni 15.

Kwa upande wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndg Kiula M Kingu amemhakikishia Mkuu wa Mkoa Usambazaji wa Maji kwa kasi kubwa na tayari eneo la Kisarawe II zoezi lilishaanza hivi wananchi wawe na mategemeo makubwa ya kupata maji safi na salama.

Mwisho ziara hiyo ya Albert Chalamila aliambatana na Viongozi waandamizi wa chama cha CCM Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Kamati ya usalama na wataalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa na DAWASA.