Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt.Pindi Chana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la Muziki wa Cigogo ambalo mwaka huu ni la msimu wa 14, tukio litakalofanyika Julai 22, katika Kijiji cha Chamwino Ikulu, Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sanaa Chamwino (CAC), Frank Mgimwa amesema mchakato wa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na vikundi 40 vinatarajiwa kutoa burudani.

“CAC tumejiandaa vyema katika kukuza na kuendeleza Utamaduni wa Mtanzania kupitia Muziki wa Cigogo wa Kabila la Wagogo ambapo mwaka huu kauli mbiu ni “Kuza Sanaa, Maadili kwanza” Ambapo vikundi vitawasilisha jumbe mbalimbali na kuonesha umahiri wao kupitia ngoma na nyimbo.

Vikundi hivi 40, kati ya hivyo 34 vinatoka Mkoa wa Dodoma  na mengine 6 yanatoka nje ya Dodoma” amesema Frank Mgimwa.

Ambapo ameongeza kuwa, vikundi hivyo sita vinatoka mikoa ya Iringa, Dar es Salaam,  Singida  na Zanzibar. 

Aidha, Frank Mgimwa amevitaja baadhi ya vikundi hivyo ni pamoja na:

Makundi ya Mkoa wa Dodoma ni Nyati, Swala, Nyota lamali, Nyerere, Ufunuo (Majeleko), Nuru, Nyundo, Ushirikiano, Jembe, Chibibi, Yeriko, Upendo, Nyemo, Ndagwa, Nyota njemana mengine mengi.

By Jamhuri