Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo akiwa Kibaha, Pwani kufunga mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa amesema anamfuta kazi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanafi Msabaha kutokana na kupeleka mradi mahali ambako haukutakiwa kwenda na kusababisha Wananchi warudishe kadi za Chama.

“Mkuu wa Wilaya anahongwa, mradi anaacha kuupeleka unakotakiwa anaupeleka usikotakiwa, kiasi kwamba Wananchi wanafikia kurudisha kadi za Chama, sisi huku tuna haja kubwa ya mradi mmetuacha mmekwenda kuupeleka kwingine, kadi zenu hizo…… sina imani na DC anayesababisha kadi zirudishwe, Mtwara”

“Mkuu wa Wilaya Hanafi (Hanafi Msabaha) namtimua leo, siwezi kustahimili kadi za Chama zinarudishwa, yeye na DED wake, Mkuu wa Wilaya yupo, DED yupo kadi za Chama zinarudishwa anaulizwa anasema ‘unajua kule wengi Wapinzani’ so what?, si Watanzania wale? hawahitaji kitu!? “ ——— amesema Rais Samia.

Itakumbukwa hivi karibuni Wananchi wa Kijiji cha Lyowa kata ya Muungano Wilaya na Mkoa wa Mtwara wamefunga Shule ya Msingi ya Kijiji hicho, Wamefunga Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji, Wamemlazimisha Mwenyekiti wa Kijiji kujiengua katika nafasi hiyo lakini pia zaidi ya Wanachama 200 wa Chama cha Mapinduzi CCM wamerudisha Kadi za Chama hicho wakishinikiza kupewa pesa za Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Milioni 560 kwa ajili ya ukamilishaji wa Shule yao ya Sekond