Na Isri Mohamed

Mtanzania Clara Luvanga anayekipiga katika klabu ya wanawake ya Al Nassr huko nchini Saud Arabia ameibuka kuwa mfungaji bora wa ligi ya wanawake nchini humo.

Luvanga ambaye klabu yake ya Al Nassr ladies imechukua ubingwa wa ligi, amefunga mabao 11 katika mechi 11 alizocheza.

Luvanga alijiunga na Al Nassr Ladies katikati ya msimu uliopita mwezi Oktoba, 2023 akitokea Spain alipodumu kwa mwezi mmoja tu.

Klabu ya Al Nassr imejizolea umaarufu mkubwa duniani kwa sasa baada ya timu yao ya wanaume kumsajili nyota wa kimataifa, Cristiano Ronaldo, na kwa upande wa hapa nchini ikijizolea mashabiki wengi kupitia Clara Luvanga.