Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA

Nyota Dario Frederico kutoka klabu ya Singida Big Stars ameongezewa muda wa likizo na timu yake hiyo baada ya kupewa likizo ya mwezi mmoja kwa akili ya matibabu nchini Brazil na ripoti ya daktari ikionesha amepona kwa asilimia 90.

Klabu imemuongezea nyota wake huyo muda ili aweze kuwa timamu kwa asilimia 100 na apate muda wa kutosha kupumzika.

kutokana na kuongezewa muda wa likizo klabu imeeleza kuwa Frederico atarejea na kujiunga na kikosi hicho wakati wa maandalizi ya ligi kuu msimu ujao (Pre-season) 2023/24 huko nchini Tunisia.

Dario Frederico alisema alirejea Brazil kwa ajili ya mambo ya kifamilia huku akiwatoa hofu mashabiki zake atarejea muda sio mrefu kuendelea na majukumu kama kawaida.

Dario Frederico alikuwa mchezaji watatu kuondoka Singida Big Stars akitanguliwa na mwenzake, Peterson Cruz na Muargentina, Miguel Escobar ingawaje wawili hao hawakuweza kurudi tena nchini kwani walipata timu nyingine.

By Jamhuri