Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA

Shirikisho la Soka Zanzibar ‘ZFF’ limewaonya Wachezaji wa Klabu za Ligi Kuu visiwani humo ‘PBZ Premier League’ pamoja na Ligi Daraja la kwanza Kanda ya Unguja na Pemba, kutojihusisha na kucheza Michuano ya Mitaani (NDONDO Cup) kwa kipindi chote cha Mapumziko ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na mawasiliano ya ZFF leo Ijumaa ya Machi 24 imeeleza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa mchezaji yeyote wa ligi hizo atakayebainika kucheza michuano isiyo rasmi kwa mujibu wa kanuni ya mashindano 2022/23.

“ZFF inawaomba Waanzilishi wa Ndondo Cup katika kipindi hichi cha Ramadhan kufuata Miongozo yote ya kanuni ya Mashindano na kutowahusisha Wachezaji wa Ligi kuu na Daraja la kwanza kwenye michuano yao hiyo.”imesema taarifa hiyo

Aidha ZFF imewataka waanzilishi wa Ndondo Cup kufuata miongozo yote ya kanuni ya mashindano ba kutowahusisha wachezaji wa ligi kuu na Daraja la Kwanza kwenye michuano hiyo kwa kipindi hichi cha Ramadhan.

Shirikisho la Soka visiwani Zanzibar ‘ZFF’ limetangaza kusimamisha Ligi zote ili kupisha ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhana, ambayo rasmi ilianza jana Alhamis (Machi 23, 2023).

By Jamhuri