Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wakazi wote wa maeneo ya Kiharaka, Kiembeni, Changuaela, Kerege, Kibosha, Mtambani na Kimele.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Machi 25, 2024 na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa ofisi ya DAWASA Mapinga inaendelea na zoezi ambapo zaidi ya wateja 100 wanatarajia kunufaika na huduma ya Majisafi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa pamoja na zoezi hilo, elimu mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji na matumizi sahihi ya maji.

“Pia itatolewa elimu kuhusu njia rasmi za mawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA. Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja nambari 0800110064 (Bure) au 0735 202121 (WhatsApp tu) 0734 359622 (DAWASA Mapinga),” imeeleza taarifa hiyo.

By Jamhuri