Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mbinga

Mkuu wa Wilaya Mbinga Aziza Mangosongo alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Mkeke, kata ya Amani Makolo, Akiwataka wananchi wote wanaoishi kwenye eneo la hifadhi ya mlima amani makolo kuondoka mara moja ndani ya siku saba, utekelezaji wa agizo hilo unaanza mara baada ya tamko hilo.

“Kwa mamlaka niliyopewa mimi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ninawaamurisha kutoka kwa hiari yenu katika eneo la msitu wa hifadhi ya amani makolo ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 16/8/2023, Tofauti na hapo nguvu ya ziada itatumika dhidi yenu, kikundi au mtu yeyote atakayekaidi amri hii atachukuliwa hatua kali za kisheria” amesema.

‘Kama wananchi mnahaki ya kuishi, kusafiri, kupata elimu, kuchagua na kuchaguliwa lakini wakati unatafuta haki hakikisha uvunji wala kukiuka sheria na miongozo iliyopo, Vilevile alitumia nafasi hiyo kuwasikiliza na kupokea kero zinazowakabili wananchi hao ikiwemo maji, miundombinu, umeme, afya na elimu” amesema.

Sambamba na hilo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi wao, kuzingatia lishe bora kwa kupata mlo kamili, Kujenga tabia ya kupima malaria na kutumia vyandarua vyenye dawa, Vilevile wazazi washirikiane na walimu kudhibiti suala la utoro kwa wanafunzi shuleni

Amemtaka Mkurugenzi kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha zahanati ya kijiji sambamba na mganga mkuu ahakikishe wazee ndani ya mwezi mmoja wapate kadi za matibabu pamoja na wazazi kuacha tabia ya kuwashawishi watoto kuacha shule kiholela.

Naye Emmanuel Samwel, Kaimu Mhifadhi Misitu Mkuu Wilaya ya Mbinga (TFS) alikiri kupokea msitu huo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya mbinga 2018, ili usimamiwe na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS),

Hifadhi ya Msitu huo inasimamiwa kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2002 ya sheria za misitu Tanzania, Kwahiyo katika hifadhi shughuli zozote za kilimo au makazi haziruhusiwi ni kinyume cha kishera, Hivyo basi ni kosa kufyeka au kulima, kuvuna, kuingia ndani ya hifadhi pasipo kibali.

By Jamhuri