Dereva wa lori aliyemgonga Twiga na kumuua katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kupata matibabu.

Hifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Ignas Gara amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Septemba 29,2022 wakati dereva huyo alikiwa akiendesha lori lenye namba T 863 AGU.

Amesema kuwa dereva huyo atatakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani elfu 15 ambazo ni sawa na shilingi milioni 34 na laki 9 za kitanzania.

Amesema kuwa dereva huyo yupo hospitali akipatiwa matibabu chini ya ulinzi wa Polisi kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo ambapo lori alilokuwa akiliendesha lilianguka kwa ubavu baada ya kumgonga twiga huyo.

Dereva huyu atakapopona atafikishwa Mahakamani baada pia ya taratibu za kisheria kukamilika.