Home Burudani Diamond Ashinda tuzo ya Soundcity MVP Nigeria

Diamond Ashinda tuzo ya Soundcity MVP Nigeria

by Jamhuri

Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ameshinda tuzo kutoka Kituo cha Runinga cha Soundcity.
Muimbaji huyo ameshinda katika kipengele cha Best Male MVP ambapo alikuwa akichuana na wasanii wengine kama Davido, RunTown, Olamide, Wizkid, 2Baba (2face) wote kutoka Nigeria na Sarkodie, Shatta Wale kutoka Ghana pamoja na Navio kutoka Uganda.


Diamond ndio msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika mashariki kushinda katika tuzo hizo.
Wasanii wengine wa Tanzania walikuwa wakiwania tuzo hizo ni Vanessa Mdee katika kipengele cha ‘Best Female MVP’ ambapo alichuana na wasanii kama Tiwa Savage, Niniola, Yemi Alade na wengineo.

Aslay naye alikuwa akiwania kwenye kipengele cha ‘Best New MVP’ ambapo alikuwa na wasanii kama Maleekberry, Mayorkun, Diceailes, SmallDoctor wote kutoka Nigeria, Na Nadia Nakai kutoka Afrika Kusini.
Wengine ni Alikiba katika kipengele cha Song of The Year kupitia wimbo wake wa Seduce Me na kundi la Nany Kenzo katika kipengele cha Best Group or Duo.

You may also like