MWENYEKITI wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dk.Titus Kamani amesema Serikali kupitia tume hiyo ni awaelekeza viongozi wa Vyama vya Ushirika kutojihusisha kuuza mali za vyama hivyo pasipo kuzingatia sheria.
 
Hivyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuuza mali za vyama hivyo na kufafanua ili kudhibiti hali hiyo Ofisi za Mrajisi wa vyama vya ushirika imekuwa ikichukua hatua ikiwa pamoja na kuwaondoa viongozi wanaokiuka sheria.
Dk.Kamani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea udhibito wa mali za ushirika na mpango wa makusanyo na mauzo ya mazao makuu matano ya kimkakati kupitia mfumo wa ushirika.
Amesema vyama vya ushirika nchini vinaendeshwa kwa kuzingatia sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.Hivyo vyama vinapaswa kuzingatia sheria wanapotekeleza majukumu yao.Dk.Kamani amesema Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaelekeza viongozi wa vyama hivyo kuwa makini kuzingatia sheria.
 
Amefafanua vyama vina haki ya kumiliki mali na kuuza mali hizo pale itakapoona inafaa kwa kuzingatia shetia iliyopo.Pia mali zinazomilikiwa na vyama zinapaswa kuwa zimerasimishwa ili kuleta uhalali wa umiliki.
Dk.Kamani amesema pamoja na uwepo wa taratibu za kisheria zinazoelekeza namna ya ununuzi ,uuzaji na urasimishaji wa mali zake,baadhi ya viongozi wa vyama wamekuwa hawazingatii na matokeo yake wamekuwa wakiingia kwenye migogoro na wanaushirika.
Amesema kutokana na uzito wa jambo hill la umiliki wa mali, mwaka 2016 akiwahutubia wananchi wa Jiji la Mwanza, Rais Dk.John Magufuli alieleza jinsi viongozi wa vyama vya Ushirika wanavyohujumu vyama na kujinufaisha.
 
Hivyo alitoa maelekezo yakiwamo ya kurejeshwa kwa mali zote za vyama vya vikuu vya Ushirika vya NCU (1984)Ltd na Shirecu (1984)Ltd zilizouzwa kinyemela ambapo kutokana na agizo hill hadi sasa kati ya mali za NCU ,7 tayari zimerejeshwa na kati ya mali 2 za Shorecu zote zimerejeshwa .
“Kwa dhati ya moyo wangu,nawashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa nchi kwa imani kubwa waliyonayo juu ya Ushirika kwa kuutetea na kuhakikisha unatumika kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini,” amesema Dk.Kamani.Amesema pia Serikali inawakumbusha wakurugenzi wa halmashauri za majiji ,manispaa ,wilaya na miji kuhakikisha vinakodi maghala kwa ajili ya kuhifadhi pamba.
Hiyo ikiwa ni maandalizi kwa vyama vya Ushirika katika msimu wa mwaka 2018/2019 kama yalivyo maelekezo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Please follow and like us:
Pin Share