Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji TIC na Mwenyekiti wa Kamati Uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wachumi Tanzania Economics Society Of Tanzania (EST) Bw. Godfrey Mwambe akipokea katiba ya Chama hicho kutoka kwa Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT)kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa jumuiya hiyo kwenye ukumbi wa BOT leo jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati anayeshuhudia ndiye aliyezinduam, Kulia ni Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati akizindua katiba ya chama hicho kwa kushirikiana na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi wakishiriki katika zoezi hilo.
Baadhi ya wachumi wakiwa katika uzinduzi wa jumioya hiyo leo kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati akionyesha katiba ya chama hicho na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wakishiriki katika zoezi hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi wakionyesha katiba ya Jumuiya hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam..
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki mbalimbali wa mkutano huo wa uzinduzi ambao ni wachumi na wanachama wa (EST)
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi walioshiriki katika uzinduzi huo.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi walioshiriki katika uzinduzi huo.
WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philipo Mpango amesema kuna baadhi ya watu nchini wamekuwa wakijidai wana shahada za uchumi lakini kiuhalisia ni mambumbu wa uchumi.

Pia amesema kutungwa kwa sera au kufanyika kwa maamuzi yasiyoendana na taaluma ya uchumi kunakopelekea kuumiza wananchi masikini kutokana na uwepo wa wachumi feki ambao wanapewa nafasi serikalini ,vyuoni hata kwenye sekta binafsi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo na nyingine iko haja nchi kuwa na jJumuiya ya Wachumi au chama hai cha wachumi na chenye nguvu kwani ni muhimu sana.Dk.Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi chama cha Jumuiya ya Wachumi (EST) ambapo ametoa sababu tatu za umuhimu wa jumuiya hiyo.

Amefafanua sababu ya kwanza tasnia ya uchumi ina nafasi ya pekee katika kazi ya kujenga nchi kijamii,kiuchumi na hata kisiasa.”Wachumi tunategemewa tuwe viongozi .Bila shaka waumini wenzangu wa John Maynard Keynes kuna maneno amewahi kuyasema na naomba nimnukuu.

Amesema hivi mawazo ya wachumi na wanafalsa wa siasa ,yawe sahihi au so sahihi yana nguvu kuliko inavyoeleweka kwa wengi.”Watu wanaojiamini kwamba wako guru na ushawishi wa wanataaluma ,kiuhalisia watu hao ni watumwa wa mchumi fulani marehemu,” amesema Dk.Mpango wakati ananukuu manneo ya Keynes.

Amesema sababu ya pili inatokana na ukweli siku za usoni hazifahamiki mia kwa mia na wao wachumi hawana anasa ya kufanya majaribio ya maisha ya watu katika maabara kama wenzao wa upande wa sayansi asilia.Ameongeza endapo watafanya majaribio na misingi ya uchumi jumla kiuhalisia bila shaka moto utawaka kwa maana ya mfumuko wa bei kupanda,thamani ya sarafu kuanguka, uzalishaji kushuka, wananchi kukosa huduma za msingi.

Pia vijana kukosa ajira na mambo mengine mengi ambapo athari zake ni kuchochea maandamano mitaani ambayo yamesabaabisha serikali nyingi kuanguka.Hivyo ili kuepuka kufanya makosa makubwa kupita kiasi mbadala wa maabara kwa wananchi ni uwepo wa jukwaa la mijadala ya kukosoana na kubadilishana mawazo kuhusu Sera na mwenendo wa uchumi wa Taifa.

Wakati sababu ya tatu,Dk.Mpango anasema ni jumuiya hai ya kusimamia kazi za wachumi hapa nchini.Matokeo take kumewepo na wachumi feki,kukosekana kwa udhibiti wa vyeti.Pia uwepo wa Stashahada na Shahada zinavyopatikana au kutengenezwa kwenye mitandao ya kompyuta na matokeo yake kuharibika kwa sofa za wachumi wazuri wa Tanzania.

“Kuna msemo unasema samaki mmoja akioza basi wote wameoza.Hivyo kupitia jumuiya hii ya wachumi naomba sana safari hii tufanye tofauti kwa kurekebisha hali hii na natumaini itakuwa no kwa mara ya mwisho.

” Baadhi yenu mtakumbuka Jumuiya ya Wachumi Tanzania kwa mara ya kwanza ilisajiliwa Novemba 15 mwaka 1996 na ikapewa hati ya usajili Juni 26 mwaka 2013 na Wizara ya Mambo ya Ndani.

“Baadhi ya malengo makuu ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kulinda tasnia ya wachumi nchini,kuwaunganisha wachumi, kusimamia weledi wa wachumi,kuhamasisha na kuimarisha utafiti na uchambuzi wa taarifa,” amesema Dk.Mpango.

Ameongeza kupitia Sera na mipango mbalimbali ya maendeleo ya Serikali kwa ujumla na kisekta na kuimarisha uhusiano na taasisi nyingine.Dk.Mpango amesema hata hivyo imepita miaka takriban 20  kuanzia mwaka 1998 hadi hivi sasa ambayo jumuiya imekuwa mfu au haionekani kuwepo au kutoa mchango wowote kwa nchi yetu kama ilivyokusudiwa.

Amesema matarajio yake kuanzia leo Tanzania itakuwa na Jumuiya ya Wachumi yenye nguvu itakayojengwa juu ya misingi ya weledi na utaalam,elimu na ujuzi,bidii,uzalendo ,uwazi na uwajibikaji.Pia anapenda kuona Jumuiya ya wachumi ambayo itajinasibisha kwa umahiri wa kukuza utafiti wa kiuchumi,maendeleo ya nchi na mafunzo ya wachumi kazini.

Amesema anataka kuona Jumuiya yenye kuratibu jukwaa la mijadala kuhusu sera za kiuchumo na maendeleo ya Taifa.Ametumia nafasi hiyo kuwatambua na kuwapongeza wachumi wazalendo ambao wameiweka nchi yetu ya Tanzania katika ramani ya dunia ya wachumi mashuhuri.

Amesema wa kwanza ni Profesa Justian Rweyemamu,wa pili ni Rais mstaafu ,Dk.Jakaya Kikwete na watatu ni Gavana mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Profesa Benno Ndulu .

“Hawa kwa maoni yangu wanastahili tuzo na napenda Jumuiya ya Wachumi mpya itafakari vigezo na namna bora ya kuwatambua na kuwaenzi wachumi hawa ,” amesema Dk.Mpango na kuongeza” Na vilevile kutambua wachumi wengine wenye sifa kama hizo na hata wachumi chipukizi ili kutambua vipaji vyao”.

 

By Jamhuri