MAKAMU wa Rais Dkt. Philip leo Desemba 10,2023 akiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma ambako ameshiriki Ibada ya jumapili ameitaka Mitandao ya kijamii nchini itumike vizuri pasipo kupotosha umma.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa mitandao ya kijamii ni mizuri na ni mibaya hasa ikitumika vibaya inapotosha umma na kutumia nafasi hiyo kuwataka isitumike vibaya.

“Ahsanteni sana kwa kuniombea yamesemwa mengi na wengine wamesema mimi ni mzuka, zaburi ya 118 aya ya 17 inasema sitakufa bali nitaishi na kuyasimlia matendo makuu ya Mungu kwa hiyo Mlmitandao ni mizuri lakini imekuwa ikitumika vibaya, wengi wamenitangaza kuwa Mzee amekata moto na vijukuu viliponiona vikanifuata, kwahiyo jitahidini kuitumia vizuri kwa kumwogopa MUNGU,” amesema Dkt. Mpango.

Amewashukuru Watanzania kwa kumuombea na kuwataka wawe na amani kwani amerejea nchini akiwa salama wa afya njema kabisa..

By Jamhuri