Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Zanzibar

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na sekretarieti ya kamati maalum, sekretarieti za Mikoa na Wilaya CCM Zanzibar katika kikao chake cha kwanza na watendaji hao ukumbi wa Afisi kuu CCM Kisiwandui tarehe: 5 Februari 2024.

Aidha, Makamu Mwenyekiti CCM Dk.Mwinyi amesema kazi kuu ya Chama cha siasa ni kushinda chaguzi za dola.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vema Chama cha Mapinduzi na kukiimarisha.

Kwa upande mwingine Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewapongeza watendaji kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuimarisha chama na kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Halikadhalika Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewataka watendaji kutoa fursa sawa kwa wagombea wote na kujiepusha kutengeneza makundi wakati wa uchaguzi.

Vilevile amewasisitiza watendaji hao wana wajibu wa kusimamia kanuni za chama kuhakikisha umoja , amani na utulivu una kuwepo ndani ya chama.

Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewataka wana CCM wote kuwa mstari wa mbele kuelezea vema mafanikio ya ilani ya utekelezaji wa CCM kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa kugusa sekta nyingi za utekelezaji pamoja na kuvuka lengo ikiwemo sekta elimu, afya , barabara, maji, uwezeshaji wa vikundi vya wajasiriamali .

By Jamhuri