Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inapenda kuzialika kampuni zote za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi kushiriki katika Duru ya kwanza .

Rais Dk.Mwinyi amewakikishia wawekezaji wote wa sekta ya mafuta na gesi kuwa Serikali iko tayari kuwahikikishia mazingira mazuri ya uwekezaji kwa manufaa ya wote.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipozindua Duru ya kwanza ya Utoaji wa vitalu kwa Kampuni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia maeneo ya baharini Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege tarehe: 20 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa dhamira ya Serikali katika uchumi wa buluu ni kuimarisha uchumi wa nchi kwa haraka na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo endelevu ya vyanzo vya nishati ya uhakika.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inaamini kuwa uchumi wa Buluu una fursa nyingi za kukuza mipango ya maendeleo ya kiuchumi yenye lengo la kupunguza umasikini na kutengeneza fursa za ajira nchini.

Please follow and like us:
Pin Share