Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko leo ameshuhudia fainali ya mashindano ya Mwl. Doto CUP 2023, wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo Walimu katika wilaya hiyo wameshindana katika  michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, Bao, kuvuta kamba na kukimbia.

Mashindano hayo yamefanyika ikiwa ni shamrashamra za kuelekea katika kilele cha Siku ya Walimu Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 5 ya mwezi wa Kumi.

Katika fainali hizo, Dkt.Doto Biteko ameshuhudia timu ya mpira wa miguu kutoka Kata ya Namonge ikishindana na Timu kutoka Kata ya Katente ambapo timu kutoka Kata ya Katente imeshinda kwa mikwaju ya penati.

Mgeni rasmi katika fainali hiyo, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella amemshukuru Dkt.Doto Biteko kwa kuandaa mashindano hayo kila mwaka ikiwa ni utamaduni wake wa kuwaenzi Walimu kutokana na mchango wanaoutoa kwa Taifa.

By Jamhuri