Dkt. Biteko na Naibu Waziri Kapinga wafanya kikao cha kimkakati

Dodoma.

Mipango ya kuboresha Sekta ya Nishati yajadiliwa

Leo Oktoba 19, 2023 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kuhusu Masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati lengo likiwa ni kuzidi kuboresha Sekta hiyo nchini ili kupata nishati ya uhakika na inayotabirika.

Kikao hicho kifupi kimefanyika katika ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Bungeni jijini Dodoma.