Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mchezaji wa Timu ya Pete ya Bunge Queens, Dkt. Tulia Ackson (katikati mbele) akiongoza wachezaji wa timu hiyo kusherekea ushindi wa magoli 53 – 24 dhidi ya timu ya Bunge la Kenya wakati wa Mashindano ya 12 ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotegemea kuhitimishwa leo tarehe 1 Disemba, 2022 Jijini Juba Nchini Sudan Kusini.
chezaji wa Timu ya Pete ya Bunge Queens na Mke wa Rais wa awamu ya Nne, Salma Kikwete akirusha mpira kuelekea golini mwa wapinzani wao ambao ni timu ya Bunge la Kenya wakati wa Mashindano ya 12 ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotegemea kuhitimishwa leo tarehe 1 Disemba, 2022 Jijini Juba Nchini Sudan Kusini.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mchezaji wa Timu ya Pete ya Bunge Queens, Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Spika wa Bunge la Sudan Kusini, Mhe. Jemma Kumba wakati akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo kabla ya kuanza kwa mechi yake na Timu ya Kenya wakati wa Mashindano ya 12 ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotegemea kuhitimishwa leo tarehe 1 Disemba, 2022 Jijini Juba Nchini Sudan Kusini.
Katika mchezo huo Bunge Queens iliibuka na ushindi wa magoli 53 – 24 dhidi ya timu ya Bunge la Kenya.