Na Isri Mohamed, JamhuriaMedia, Dar
Mshambuliaji Prince Mpumelelo Dube raia wa Zimbabwe, kupitia ukurasa wake wa instagram ametangaza rasmi kuachana na klabu ya Azam FC, baada ya kudumu klabuni hapo kwa miaka minne.
Hivi karibuni Azam FC walitoa taarifa ya mshambuliaji huyo kuomba kuachana na klabu yao, na kuweka wazi kuwa hawamzuii kuondoka isipokuwa utaratibu wa kimkataba ufuatwe.
Jana kwenye mechi yao dhidi ya Coastal Union [FT 1-1] Dube hakuwa sehemu ya kikosi na leo asubuhi ametangaza kuondoka Klabuni hapo
Hii ni ishara kwamba kila kitu kimeenda sawa kati yake na klabu, lakini bado upande wa Azam hawajatibitisha kwamba tayari wameshamalizana nae.