Na Isri Mohamed, JamhuriMedia

Bodi na Menejimenti ya Klabu ya Singida Fountain Gate FC imefikia uamuzi wa kuvunja benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu Thabo Senong, kufuatia mfufulizo wa matokeo yasiyoridhisha ya klabu hiyo.

Mechi tano za mwisho Singida FG wamepoteza mbele ya Mtibwa Sugar, Azam FC, Tanzania Prisons, Kagera Sugar na kupata sare dhidi ya Tabora United.

Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Singida Fountain Gate, Hussein Massanza imesea uongozi utatangaza benchi jipya la ufundi muda wowote kutoka sasa.

By Jamhuri