Nchi wanachama wa Nchi za Afrika Mashariki zimekubaliana kuja na mkakati wa miaka mitano ya kupunguza taka za kieleketroniki na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wa nchi hizo ya namna bora ya kukabiliana na taka hizo ikiwemo kuteketeza na kuzitupa eneo husika.

Ameyasema hayo leo Machi 22,2023, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO) Dkt Ally Simba wakati wa Ufungaji wa Mkutano uliondaliwa na EACO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi saba za Afrika Mashariki kujadiliana kwa pamoja namna ya kukabiliana na taka zinazotokana na vifaa vya kielektroniki.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo akifunga Mkutano uliondaliwa na EACO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi saba za Afrika Mashariki kujadiliana kwa pamoja namna ya kukabiliana na taka zinazotokana na vifaa vya kielektroniki. Mkutano huo umefungwa leo  Machi 22,2023 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Dkt Simba amesema mkutano huo wa siku tatu umeweza kufanikisha kuja na maadhimio hayo ambayo pia yatashirikisha wanaozalisha bidhaa za kielektroniki ikiwemo makampuni husika kwa hizo nchi zote ambapo itaandaliwa miongozo husika.

Aidha amewasihi wananchi kutokukaa na taka za eletroniki kwani zimadhara hivyo kuzifikisha sehemu husika.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo amesema kuwa kama nchi kuna sheria na taratibu ambazo zimeshachukulia na zitakazotumika kuendesha namna bora ya ukusanyaji wa taka za kielektroniki.
Amesema kuwa hatua nyingine ni kuendelea kuweka msisitizo wa namna bora ya kuwaelimisha wanachi wa maeneo yote.

Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta TCRA, Dkt.Emanuel Manasseh amesema kuwa kongamano hilo limekuwa chachu na limekuwa na idadi kubwa ya waliohudhuriwa kupitia njia ya kawaida na ya kimtandao kutoka Nchi wanachama wa nchi za afrika mashariki.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO) Dkt Ally Simba
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO) Dkt Ally Simba

By Jamhuri