Baada ya kuingoza Taifa Stars kwenda suluhu ya kutofungana na Uganda The Cranes katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019, Kocha Emmanuel Amunike amekwea pipa kuelekea Hispania.

Amunike ameondoka nchini na shirika la ndege ‘Qatar Airways’ kuelekea nchini huko kwa mapumziko kabla ya kurejea tena Tanzania kwa kuanza maandalizi ya kuiandaa Stars kuelekea mechi dhidi ya Cape Verde.

Kocha huyo atawasili tena nchini kuanzia Septemba 22 tayari kwa kambi nyingine maalum ambayo itaanza Oktoba 1 kuelekea mechi hiyo ya kufuzu AFCON.

Stars itacheza na Cape Verde Oktoba 10 kuendelea na harakati za kuwania tiketi za kucheza AFCON mwakani.

Please follow and like us:
Pin Share