Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamelazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wake, Ndanda FC.
Hii ni sare ya kwanza kwa Simba baada ya ushindi mara tatu mfululizo.
Simba walishambulia mara nyingi zaidi lakini Ndanda wakiwa nyumbani Nangwanda Sijaona walikuwa makini huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza.
Washambuliaji wa wawili tegemeo wa Simba, Meddy Kagere na Emmanuel Okwi walilazimika kupumzishwa kutokana na ugumu wa mechi hiyo.
Huku kiungo mpya wa Simba, Cleotus Chama wa Azam akiichezea timu yake kwa mara ya kwanza.
Please follow and like us:
Pin Share