Na Helena Magabe JamhuriMedia, Tarime

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha Demokrasia na na (CHADEMA), Esther Matiko amesema atagombea ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini 2025 kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu baada ya kupokea maoni kutoka kwa watu mbalimbali wakimtaka agombee.

Amesema bado ana wito na ana deni la kuwatumikia wananchi kwa kuendelea kutimiza ahadi zake pamoja na kukamilisha miradi aliyoiomba akiwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini.

Anasema jambo kubwa linalomvutia na lililomfurahisha na kuamua kuendelea kugombea tena ubunge wa jimbo hilo ni kumalizika kwa mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu kati ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) na wananchi .

Mgogoro huo uliodumu kwa miaka mingi akiwa Mbunge viti maalumu hadi kuwa mbunge mwaka jana wananchi kulipwa fidia na Jeshi kuchukua ardhi.

“Mgogoro huu ni wa muda mrefu sana tangu nikiwa mbunge wa viti maalum nilianza kuufuatiki ikashindikana nikawa mbunge wa Jimbo la Tarime tena huku mwishoni ndio unamalizika na wananchi kulipwa fidia jambo ambalo limenifurahisha sana na kunipa ari ya kuamua kugombea tena” anasema.

Matiko anasema akiwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini na Halmashauri ikiongozwa na CHADEMA kupitia aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hamisi Nyanswi waliandika proposal nyingi (maandiko mengi ya miradi) likiwemo la soko la kisasa , kutenga eneo jipya la makaburi, kuzibua barabara mpya nyingi kuna maeneo yalikuwa na changamoto kwa sasa njia zinapitika pamoja na kununua eneo la dampo.

Anasema alifanikiwa kujenga Kituo cha Afya Magena, Zahati Nkongore pamoja na Kenyamari kwa ushirikiano ingawa ina suasua na kuongeza kuwa kwenye sekta ya elimu alijitahidi kujenga madarasa kwa kushirikiana na wananchi wakichagia na bado anaendelea kusukuma maendeleo.

Mafanikio mengine ni kuweka lami kwenye barabara kilometa sita na kujenga kuzunguka eneo la Tarime Mjini ambapo wataanza na kilometa 4.2 hivyo Mji wa Tarime utakuwa wa kisasa zaidi.

Si hayo tu anasema kuwa amefanikiwa kubuni mnada wa Magena ambao ulizinduliwa na aliyekuwa Waziri wa Uvuvi, Mashimba Ndaki ambao hivi sasa unatekelezwa.

Anasema kuwa baada ya kukamilika hayo sasa kinachofuatia ujenzi wa dambo la kisasa kwenye eneo jipya Magena walilonunua na kuligawa na kuhamisha lililopo mjini katikati ya makazi ya watu katika Kata ya Nyamisangura ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Kuhusu changamoto ya maji amesema imekuwepo kwa muda mrefu na aliiongelea sana kwenye kampeni na aliendelea kupigania bungeni upatikanaji wa maji safi na salama ambapo wamepata mradi wa shilingi Bilioni 134 kutoka ziwa Victoria.

Amesema katika masuala ambayo katika uongozi wake wameyaandika ni pamoja na ujenzi wa stendi ya Kemange andiko ambalo aliliandika kwenda (World Bank) Benki Kuu ya Dunia ambapo Bmbenki hiyo imeleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo itayokuwa ya kisasa.

Kuhusu malalamiko ya kushindwa kujenga shule ya msingi ya ghorofa aliyoiahidi amesema nia ipo sana ila ni matakwa na maagizo ya Serikali kutoruhusu kufatia kutokuwepo na mwongozo wa ujenzi wa wa ghorofa kwa shule za msingi.

Matiko azomewa

Akizungumzia kitendo cha kuzomewa na kikundi kidogo cha watu kwenye mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa uliofanyika February 28 alipopewa nafasi ya kuzungumza anasema hatua hiyo haikayishi tamaa kwani anaamini kuwa waluofanya hivyo si wapiga kura wake.

Anasema licha ya kuwa alizomewa na kuvunjwa moyo lakini alijitadi kuzungumza na changamoto zilizosalia aliziaandika akampatia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivyo ana uhakika changamoto hizo zitafanyiwa kazi.

Anasema kuwa kitendo hicho amekiita ni utovu wa nidhamu mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa kwani mkutano ulikuwa wa kiongozi huyo mkubwa na si wake yeye na wananchi.

Anasema kitendo hicho kilimfanya atambue ni kiasi gani ana nguvu na uwezo mkubwa hivyo ni tishio kwa waunda njama za kumzomea lakini anaaema kuwa kwa kitendo hicho hakimyumbishi na yuko imara sana .

Anaongeza kuwa katika mkutano huo wabunge walipewa dakika tano tu za kuzungumza hivyo kwa nafasi hiyo ndogo ilitakiwa mbunge aitumie kuongelea mambo ya msingi kwa wananchi .

Katika mkutano huo alimweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa ana kero zaidi ya tano za Mji wa Tarime ambapo alitoa shukrani kwa Serikali kuwalipa fidia wananchi katika mgororo wa ardhi na JWTZ uliodumu miaka mingi.

Pia aliishukuru Serikali kwa kuwalipa fidia wananchi wa Kinyambi na Bugosi waliokuwa na mgogoro wa ardhi baina ya Jeshi la Wananchi (JWT) toka 2007 hatimaye mwaka jana walilipwa fidia na kumwomba Waziri Mkuu kufikisha kufikisha shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Hasan Suluhu.

“Kwanza kabisa naishukuru Serikali kwa kuwalipa fidia wananchi wa Kinyanbi na Bugosi walikuwa na mgogoro wa ardhi toka 2007 na JWTZ wamekuja kulipwa mwaka jana naomba unifikishie shukrani zangu kwa Rais Samia” anasema Matiko.

Baada ya hapo alimshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kuweka jiwe la msingi kwenye soko la Kimataifa Tarime soko ambalo anasema waliliandikia andiko toka 2017 na hatimaye linakaribia kukamilika.

Matiko akazungumzia sekta ya elimu na kusema kuwa anatambua juhudi za Serikali kwenye sekta ya elimu, lakini elimu kwa Tarime bado miundombinu ni duni.

Akaanza na shule mbili za sekondari Mogabiri ambayo alisema ni ya muda mrefu akaiombea kuwa High school (advance) iwe na kidato cha tano pamoja na kidato cha sita.

Sekondari ya Nyabisese ambayo ni ya kutwa aliomba ipate hosteli yaani ijengewe mabweni ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya mwendo mrefu.

Kwa upande wa shule za msingi anasema kuna msongamano wa wanafunzi mfano Rebu Shule ya msingi ina wanafunzi 2060, Mturu 1900 pamoja na Buguti 2900 .

Shule nyingine alizozitaja zenye wanafunzi wengi ni pamoja na Turwa, Buhemba pamoja na Rosonti hivyo akaiomba Serikali kuongeza fedha kupitia fedha za Boost kuongeza shule za msingi ili wanafunzi wasome kulingana na uwiano unaotakiwa.

Hakuishia hapo alingumzia jinsi hosptali ya Mji Tarime inavyoelemewa na wagonjwa akasema fedha za Basket Fund zinaletwa kwa vigezo vitatu wingi wa watu, umaskini pamoja na watoto wa miaka mitano.

Akaiomba Serikali inapoleta pesa izingatie bajeti ilete fedha nyingi kwani watu wamekuwa wakitibiwa kwa kuzingatia vigezo vinavyotolewa hivyo mahitaji ya dawa hayatoshi mfano 2023 kina mama wa Tarime Mji 1050 walijifungua na vijijini 400.

Akamalizia na eneo la mlima Nkongore lenye zaidi ya hekali 100 ambalo aliomba lirudishwe kwa wananchi toka kwa Jeshi la Magereza walitumie kwa shughuli kilimo.

Akitoa majibu ya maombi hayo, Waziri Mkuu Majaliwa anasema kuwa, msongamano wa wagonjwa Hosptali ya Tarime Mjini, anasema kuwa Serikali inaendelea kumaliza msongamano kwa wagonjwa kwa kuongeza hosptali.

Waziri Majaliwa alisema 2018 alikuja Tarime alishuhudia wingi wa wagonjwa na namna madaktari walivyokuwa wakifanya kazi ngumu kuwahudumia wagonjwa lakini kwa sasa Serikali imeboresha huduma za afya kila Halmashauri.

Aidha alisema fedha zinapoletwa kila baada ya miezi mitatu Mganga Mkuu wa Hosptali ya Wilaya (DMO) anapata mgawo kwenye hospitali yake hivyo anapaswa kutoa mgawo kwenye hospitali ya Mjini maana fomu inakuja na ratiba jumuishi zikiwemo zahanati na vituko vya afya.

Kuhusu kuomba shule zipandishwe hadhi alisema maamuzi ni ya Halmashauri akashauri watengeneze vigezo kwa shule wanayoitaka waiombee.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Esther Matiko ni Mbunge ambaye ni mtetezi wa haki za binadamu katika mkutano wa Sirari Tarime Vijijini hakusita kutetea wananchi ambapo alisema kuwa jitihada zake zinaendelea.

Alimweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa pamoja na kuwa mpaka wa Sirari ni fursa ya biashara lakini wafanyabiashara wa Tarime Vijijini pamoja na Mjini wanauwa.

Alisema ni vema elimu itolewe aidha ya kikodi ili wafanyabiashara watii sheria na wakikamatwa na magendo wapigwe faini lakini sio kuuwawa.

Matiko pia aliomba Mji wa Sirari kupata Mamlaka ya Mji mdogo jambo ambalo liliwafurahisha wakazi wa Sirari na kumshangilia Waziri Mkuu Majaliwa.