

Na.Mwandishi Wetu-Nzega
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, imekutana na Watendaji Kata na Mitaa pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, leo tarehe 30 Septemba 2026 kwa lengo la kuwapa elimu kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Ndg. Shomari Mndolwa, ameishauri EWURA kuendelea kuweka mifumo imara ya udhibiti inayozingatia na kulinda maslahi ya watoa huduma na walaji huku ikitoa huduma za udhibiti zinazolenga kutekeleza Dira ya Taifa ya 2050.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally, ameeleza kuwa viongozi wa serikali za mitaa ni daraja na nguzo muhimu katika utekelezaji wa shughuli za kiudhibiti zinazohusisha utaoaji wa leseni, vibali na utatuzi wa malalamiko kati ya watoa huduma na wateja.



