#Kaya 55 zakosa mahali pa kuishi

Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Simanjiro

Mwekezaji mzawa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone Mining inayomiliki Kitalu C Onesmo Anderson Mbise wa machimbo ya Tanzanite katika Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ametoa msaada wa vyakula vyenye thamani ya sh.mil.31 kwaajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko ya Kata mbili za Simanjiro.

Kampuni ya Franone Mining LTD inayomiliki kitalu C katika machimbo ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imetoa msaada huo kufuatia mafuriko yalisababishwa na Mvua kubwa na kupelekea wananchi wa kata ya Shambarai wapatao 236 kuathirikana mafuriko hayo na huku kata Kaya 55 kutoka Kata hizo mbili kukosa Mahali pa kuishi.

Aidha Kata ya Shambarai kuna jumla ya Wananchi wapatao 236 wameathirika na Mvua huku kaya 26 kati ya 55 zikikosa Makazi ya kuishi, wakati kata ya Msitu wa Tembo kuna kaya 49 zimepatwa na maafa hayo na kusababisha Kaya 29 kati ya hizo 55 kukosa Makazi ya kuishi.

Kufuatia hilo Kampuni ya Franone Mining Onesmo Mbise imeweza kutoa msaada wa vyakula kama mahindi gunia 200, maharage gunia 40, Sukari mifuko 20 na mafuta ya kula katoni 40 ili kuweza kuziiwezesha Kata hizo kupata chakula cha kujikimu katika maisha hayo magumu wanayopitia.

Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone Mining Onesmo Anderson Mbise pamoja na Mkurugenzi mwenza Francis Joseph Matunda pamoja na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Vitus Ndakize walikabidhi vyakula hivyo Kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Suleiman Serera, akiwepo Mbunge wa jimbo hilo Christopher Ole Lekaita, baadhi ya adiwani wa kata na viongozi mbalimbali.

” Sisi kama Kampuni ya Franone Mining tunaifanya kazi katika Wilaya ya Simanjiro na Mkoa wa Manyara tunashirikiana na jamii katika nyanja mbaliiiii katika wakati wa Raha nawakati wa shida, nimkweli Mvua hizi zilizonueaha zilileta madhara makubwa sehemu mbalimbali hapa Nchini , ambapo tumepata taarifa kutoka kwako Mkuu wetu wa Wilaya kuwa tumepata shida katika kata ya Shambarai Kijiji Cha Kilombelo na Kata ya Msitu wa Tembo, ambapo sisi kama Kampuni tulikaa tukazungumza na tukaona tutafute chakula kidogo tulete hapa namleo hii tumeleta Mahindi gunia 200, maharage gunia 40, Sukari mifuko 20 na mafuta ya kula katoni 40, ambavyo vyote vina thamani ya sh.mil. 31″ alisema Mkurugenzi Mbise.

” Hiki ndicho tulichokipata na tulichojaaliwa na Mwenyezi Mungu kuleta hapa, sasa huko mbele ya safari kadri tutakavyoendelea kushirikiana hali itakavyoturuhusu basi tutaendelea kulingana mkono” aliongea Mkurugenzi huyo

” Mh.Mkuu wa Wilaya sisi kama kampuni ya Franone tunashirikiana na jamii inayotuzunguka ndiyo sababu ulipotuambia watu wa Msitu wa Tembo na Shambarai wamepata maafa tukaona tusaidie vyakula hivi,” amesema Mbise.

Naye Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Dkt Suleiman Serera, ameishukuru kampuni ya Franone Mining kwa kutoa msaada huo wa wahanga wa mafuriko yaliyotokeakatika Kata hizo mbili, ambapo amesema kufanya hivyo kutawasaidia katika kupata matumaini ambayo yalianza kupotea juu yao.

” Niwashukuru sana sana wenzetu wa Kampuni ya Franone Mining Kwa msaada huu mkubwa mliotukabidhi hii Leo, mmetukimbilia mmetusaidia kutupatia chakula, niwashuru sana wadau wetu kwa naiba ya Serikali, hata Mh.Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan amekua akitoa Rai kwa wadau wote waweze kutoa misaada, ninyi mmewahi mmetukimbilia na hii ndio dhana ya kutoa kwa jamii, hii ni sehemu mojawao ya kutoa kwa jamii sio fedha tu kwamba ndio ziende waonekane lakini inapotokea changamoto Badi msaada huo ukatolewa kwa ajili ya wenzetu hio ndio kukimbiliana, kukimbiliana kupo, ukampa chakula, hata Mwenyezi Mungu naye anaweza kuweka ama kufanya jambo fulani, kwahiyo kwaniaba ya Serikali niseme tu kuwa tunawashukuru sana Kwa hiki ambacho mmetuletea, licha ya kuwa baadhi ya wahanga nyumba zao zimebomoka kupitia mafuriko hay na wengine vyakula vyao vimetoweka na kuharibiwa na Mvua ila watapata ahueni kupitia msaada huo wa Franone Mining, Mwenyezi Mungu aendelee kuwabariki sana, ameongeza Mkuu hiyo wa Wilaya.

Aidha Mkuu huyo amebainisha maeneo yalioathirika zaidi katika kata hizo Wilayani Simanjiro kuwa ni Vijiji vitatu katika kata ya Shambarai ambacho ni Kijiji Cha Shambarai chenyewe, Kilombero na Orbili na katika kata ya Msitu wa Tembo ni Kijiji Cha Msitu wa Tembo na kijiji cha Londoto.

Aidha Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ameipongeza kampuni ya Franone Mining kwa kuweza kutoa chakula hiko kwa waathirika wa mafuriko hayo amblo ni jangahilo ni kubwa linalotakiwa kuiunga mkono na Mwananchi yeyote yule ili kuunga mkono jitihada na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.

Mbunge Sendeka amesema janga hilo lililopotea Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Suleiman Serera akifanya Mawasiliano ya Mkugenzi wa Franone Mining ili kuweza kusaidia hilo tatizo, ambapo naye alipataka kumweleleza Mkurugenzi huyo alijibiwa kuwa tayari wameshapata maombi kutoka Kwa Mkuu wa Wilaya hiyo.

” Kwa namna ya pekee ndugu yangu Onee npamoja na wakurugenzi wenzako na watumishi wote wa Kampuni ya Franone Mining nichukue nafadi hii kuwapongeza sana, sio tu kuwashukuru kwa ajili ya hili, kwakweli ninyi mara nyingi mekuwa msaada mkubwa kwa jamii kndio maana nasema tunawashukuru Kwa mengi” amesema Mh.Sendeka.

Sendeka alisema Kampuni ya Franone Mining hivi karibuni waliweza kuwashika tena mkono wakati wa kiangazi ambapo walizisaidia shule mbili katika kata ya Naisinyai, shule ya Msingi Naisinyai yenyewe pamoja na Oloshonyokie Kwa kuwapatia Mahindi gunia 120, maharage gunia 20, pamoja na mafuta ya kupikia ndoo 20 za Lita 400.

” Mmetushika Mkono katika jitihada mbalimbali, ambapo pale mlipoombwa msaada na wananchi wetu mmekua mkiwadaidia mara zote, nilikua napiga mahesabu tu haraka haraka hapa ni zaidi ya sh.mil.mil. 140 hivi katika kumbukumbu zangu ambazo mmetuchangia katika shughuli mbalimbali za Maendeleo kwatika jamii kwa mara zote, hakika mawapongezeni sana sana kwa Moyo wenu wa kiungwana.

” Hata kule Hanang niliwaambia Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga na Jenista Mhagama na Waziri wa Madini Antony Peter Mavunde kwamba tunawaomba Kampuni ya Franone Mining tumewaomba watusaidie kubeba mzigo mkubwa tulionao kule Simanjiro kwa mafuriko haya iwapo hamtawaona Franone Mining huku Katesh, mjue kabisa wao ndio pekee yao waliobeba mzigo wa kusaidia maafa ya Kata hizi mbili na Leo mmeshuhudia hapa magunia yote mliyoyaona hapa yametokea Kampuni ya Franone Mining, Kwa hiyo ngudu yangu wakurugenzi wa Kampuni hii nawashukuru sana Kwa Moyo wenu wa kutukimbilia wakati wote wa changamoto hizi.

Aidha alisema kufanya hivyo ni kumuunga Dkt.Samia Suluhu Hassan katika jitihada ambazo amezifanya hususani alipomwelekeza Waziri Mkuu aelekeze nguvu zote Hanang katika kuwahamasisha jamii, Taasisi za Umma, ili wachangie na hatimaye kuisaidia Hanang iliyokuwepo kwenye matatizo ya maafa katika Wilaya ya Hanang, hivyo ameipongeza Kampuni ya Franone Mining Kwa kuunga mkono mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Asia Ngalisoni amewashukuru wadau hao wa Maendeleo wa Kampuni ya Franone Mining kwa kutoa msaada huo ajili ya waathirika wa maafa hayo, ambapo amesema waliokumbwa na mafuriko ni watu 236 katika kata ya Shambarai, na katika Kata ya Msitu wa Tembo kwenye kaya 49 zimeathirika na maafa hayo.

” Kwa niaba ya Mkugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Gracian Makota nawashukuru na kuwapongeza sana wakurugenzi wa Kampuni hii ya Franone Mining Kwa kutoa msaada huuwa chakula, mmetuthamini, mmetujali mmefanya Kwa niaba ya Halmashauri, kitendo hiki tulitakiawa sisi Halmashauri tukibebe Kwa ajili ya Wananchi , lakini ninyi mmeona umuhimu wa kuiisaidia jamii yetu, tunawashukuru huu” amesema kaimu Mkurugenzi

“Mchango mlioutoa na tutaendelea kuhakikisha tunasimamia wanachi waliopata na maafa kama vyakula hivi vilivyotolewa, hata Mh.Rais juzi alisema michango hii inayotolewa na wadau ihakikishwe inawafikia wananchi ambao ni walengwa na si vinginevyo, nikuahidi Mh.Mkuu wa Wilaya, Mh.Mbunge, Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi wa Franone Mining msaada huu utaenda kuwafikia walengwa wote waliokusudia na si vinginevyo” ameongeza Asia Ngalisoni.

By Jamhuri