Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wananchi katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ugawaji wa vitambulisho kwa umma unatarajia kuanza tarehe 12/12/2023 katika wilaya zote za mkoa huo.

Hivyo, wananchi wote waliosajiliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa (NINs) mnaombwa kujitokeza na kuchukua vitambulisho katika ofisi za Serikali za mitaa, ndani ya siku kumi na nne (14) tangu kuanza kugawiwa kwa vitambulisho hivyo ndani eneo husika .

Mwananchi atakayeshindwa kuchukua Kitambulisho chake ndani ya muda uliopangwa katika eneo lake, atalazimika kukifuata Kitambulisho chake katika ofisi ya NIDA ya Wilaya anayoishi.

Usomapo au kusikia tangazo hili tafadhali mjulishe na mwingine.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Barabara ya Kilimani, S.L.P 12324, Dar es Salaam, Simu: +255734220962,

Barua pepe: [email protected], Tovuti: www.nida.go.tz

By Jamhuri