Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

Serikali imezindua kampeni ya Kitaifa ya elimu ya mmonyoko wa maadili ambayo itafanyika kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Juni hadi Desemba mwaka huu huku akiwataka wazazi na walezi kufanya  vikao vya mara kwa mara na watoto wao ili kuondoa changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Akizindua muongozo huo ambao ulienda sambamba na maadhimisho ya siku ya familia duniani Waziri wa maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dk.Doroth Gwajima amesema jamii lazima iwe na utaratibu wa kukaa na watoto kuzungumzia masuala ya maadili.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Kimataiafa ya familia,yaliyofanyika leo   Mei 15, 2023  katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Amesema,”katika kuhakikisha tunapinga kwa nguvu mmonyoko wa maadili  tunaoushuhudia sasa siku ya leo nitazindua kampeni maalumu kampeni ya kitaifa ya elimu  ya mmomonyoko wa maadili ambayo itafanyika kwa kipindi cha miezi sita ambapo tutaenda kufika hadi katika ngazi ya chini,”amesema

Katika hatua nyingine Dk.Gwajima amesema vitendo ya ukatili vimeongezeka kutoka visa 11,499 mwaka 2021 hadi kufikia visa 12,123 mwaka jana.

Amesema mikoa kinara  kwa vitendo vya ukatili  ni Arusha, Mbeya, Kinondoni, Tanga na Mwanza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Fatma  Taufiq  alisema jamii ikiwa na malezi na makuzi bora masuala ya ukatili hayatakuwepo huku akisisitiza kila mtu kwa imani yake  kumrudia mwenyezi mungu.

Amesema  kama jamii itazingatia maadili mema  familia zitakuwa na amani na tukikengeuka watakaoumia zaidi ni watoto hivyo kila familia ni budi kuwa na upendo .

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya familia jijini Dodoma, Mei 15, 2023.

“Tunamshukuru Rais Dk.Samia Kwa namna ambavyo anafanya kazi ya kupeleka maendeleo Kwa wananchi na leo tumekutana hapa Kwa ajili ya kujadili jambo la mwingi ambapo tunasisitiza wanafamilia kujenga ustawi na kuendelea kuikumbusha jamii kuwa wajibu wa kuitunza familia ni wa  kila mtu.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo John Jingu alieleza kuwa maadhimisho ya siku ya familia kimataifa,inatokana na maadhimio ya kimataifa tangu 1993 likitaka mataifa yote kufanya siku ya familia kila Mei 15.

Amesema siku hii hutumika kutafakali namna ya kufanya malezi na kauli mbiu ni imarisha maadili na upendo Kwa familia imara.

Kwa upande wake Naibu Waziri WA Kilimo ambaye pia ndiye Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema familia ni taasisi muhimu kwa ajili ya ustawi wa jamii .

Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Mrakibu msaidizi wa Polisi Dk. Ezekieli Kyogo,akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya familia jijini Dodoma, Mei 15, 2023.

“Leo ni siku muhimu kuhakikisha tunaishi katika maadili kuwalea na kuwatunza watoto.Dodoma kuna wakati tulipata ya kuwa na watoto wengi wa mitaani ukiwauliza changamoto yao ni kutoluelewana na familia siku ya leo tutapata fursa ya kuelimisha jamii kuhusu suala la malezi Bora.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa salaam za mkoa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Familia Mei 15, 2023 jijini Dodoma.
Wananchi waliojitokeza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia wakifuatilia matukio mbalimbali katika maahimisho hayo jijini Dodoma, Mei 15, 2023

By Jamhuri