Man City yakaribia ubingwa ligi kuu ya England

Klabu ya Manchester city jana Jumapili wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Etihad walifanikiwa kuchomoza na ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea bao lilifungwa na Bernardo Silva Dakika ya 46 kipindi cha pili cha mchezo.

Ushindi huo Manchester City umezidi kuwaimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England kwa kujikusanyia alama 78 wakifuatiwa na klabu za Liverpool alama 60, Manchester United alama 59,Tottenham Hotspurs alama 58, Tottenham alama 53,huku klabu za West Bromwich Albion,Stoke city na Crystal Palace zikiendelea kushikiria nafasi za mwisho.

Katika mchezo mwingine Brighton wakiwa ni wenyeji wa Arsenal walifanikiwa kupata alama tatu kwa ushindi wa mabao 2-1, Magoli ya Brighton yakifungwa na Lewis Dunk pamoja na Glenn Murray huku bao la Arsenal bao lao la kufutia machozi likifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang.

Ligi hiyo ya England inaratarajia kuendelea tena leo jumatatu kwa mchezo mmoja ambapo Crystal Palace wanawakaribisha Manchester United

Please follow and like us:
Pin Share