Afisa mkuu wa kundi la Hamas, Sami Abu Zuhri ameihimiza Marekani kuishinikiza Israel kusitisha vita vyake katika Ukanda wa Gaza kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo Nje wa Marekani Antony Blinken.

Abu Zuhri ameongeza kuwa Hamas iko tayari kukubaliana na mpango wowote utakaofanikisha kukomeshwa kwa vita.

Kauli hii inajiri wakati Blinken anatarajiwa kufanya ziara yake ya nane Mashariki ya Kati akianzia Misri kabla ya kuelekea Israel leo Jumatatu, ziara inayolenga kuhakikisha kwamba vita havitanuki hadi Lebanon.

Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani anatarajiwa kukutana na Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri mjini Kairo na baadaye Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant mjini Tel Aviv.

Ziara hii ni ya kwanza ya Biden tangu Rais  Joe Biden kutangaza pendekezo la kusitisha mapigano mnamo Mei 31.

By Jamhuri