Na Magrethy Katengu,Jamuhuri Media Dar es Salaam

Mwimbaji bongo fleva jina halisi Rajab Abdul hupendelea kujiita pia” Konde Boy” Staa Harmonize Mei 25,2024 anatarajia kuzindua album yake ya tano katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambayo ameipa jina la ‘Muziki wa Samia’ akiwa na lengo kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mei 20,2024 Harmonize amesema album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hivyo baada ya album hiyo atapumzika na (kurefresh) huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena.

Harmonize amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku pekee sana kwa Watanzani kutakuwa na mialiko na hakutakuwa na viingilio.

“Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia

By Jamhuri