Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

Baada ya vuguvugu kupamba moto kwenye mitandao ya kijamii, hatimaye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba sc, Salim Abdallah ‘Try Again’ ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu hiyo.

“Sisi kama viongozi Imefikia hatua sasa tuiokoe Simba SC, mtu pekee ambaye naona anaweza kuitoa hapa Simba na kuipeleka mbele ni Mohamed Dewji, sijui kama ataridhia ila nimemuomba arudi kuwa mwenyekiti wa bodi” amesema Try Again

Mwaka 2017 Try Again alishika nafasi ya kaimu Rais wa Simba, baadaye akawa Mjumbe wa bodi na kisha mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.