Na Isri Mohamed

Klabu ya soka ya Ihefu (Singida Black Stars) imeutangazia uma kuwa imefikia makubaliano na kocha Patrick Aussems raia wa Ubelgiji kuwa kocha wao mkuu kwa msimu unaofuata wa 2024/25.

Taarifa ya klabu hiyo inaeleza kuwa kocha huyo wa zamani wa Simba SC amesaini kandarasi ya awali ya mwaka mmoja mpaka 30 June, 2025.

Kwa taarifa hiyo ni kuwa kocha huyo atachukua mikoba ya Mtanzania Mecky Mexime.

By Jamhuri