Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mwekezaji na Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji amewapigia simu wajumbe wa upande wake akiwataka waandike barua za kujiuzulu kwa lengo la kuunda safu mpya ya uongozi.


Baada ya wajumbe kupokea simu hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameonekana kutoridhishwa na uamuzi huo na hivyo kugomea agizo hilo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimetuambia kuwa ni Try Agian pekee ndiye amegomea agizo hilo la kiongozi wao ambaye ndiye aliyewateua huku wakihoji mambo kadhaa bila majibu,

“Hadi sasa Try Again hajaandika barua lakini wengine wote tayari kama mambo yataenda sawa leo au kesho Barbara Gonzalez atatangazwa kuwa Mwenyekiti na huku Mipango ya kumpata CEO ikiendelea,”

Kwa Upande wa viongozi waliopitishwa na wanachama kwenye mkutano mkuu wanaendelea na majukumu yao kama kawaida, Kimesema chanzo hicho,

Wajumbe hao wa bodi waliokuwa chini ya Mwenyekiti Salim Abdallah ‘Try Again’
ni Dk Raphael Chegeni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.

By Jamhuri