Leo saa kumi alfajiri mtambo wa kuchoronga umeanza kazi rasmi ya utafiti wa Helium katika bonde la Rukwa.

Inaaminika kwamba reserve ya Helium iliyopo mkoani Rukwa ni ya tatu kwa uwingi Duniani nyuma ya Marekani na Qatar,utafiti huu utatupa picha halisi lakini pia utaiweka Tanzania kwenye ramani ya Dunia kama mzalishaji mkubwa wa Helium.

Gesi ya Helium ndio hutumika kwenye vifaa vya ki-eletroniki kama Simu janja(smart phones),viyoyozi,computer, na pia inatumika kwenye kifaa muhimu cha matibabu cha Magnetic Resonance Imaging(MRI).

Kazi nzuri ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji imetufikisha hapa tulipofika na mwanga tunauona wa kukua kwa sekta ya madini kwa kiwango kikubwa na kuchangia uchumi wa Taifa letu Tanzania.

Ni mapinduzi makubwa sana katika sekta ya madini,safari inaendelea kwa kasi kubwa sana.